Sunday, February 17, 2013

RAMA PENTAGONE AJIUNGA NA TWANGA PEPETA

Twanga Pepeta kisima cha burudani imeongeza utamu katika kundi lake kubwa kwa kumpokea Rama Pentagone aliyeacha kundi la X-tra Bongo hivi karibuni na kujiunga na kundi hilo kongwe.

BAADA YA KIFO CHA SUSAN 'GOLDIE' HARVEY MAKUBWA YAFUMUKA


Andrew Harvey na Goldie

Siku ya Harusi
Baada ya kifo cha Susan Oluwabimpe Harvey maarufu kama  Goldie siri kubwa yafumuka. Pamoja na Prezzo kudai kuwa angemuoa Goldie taarifa zenye uhakika ni kuwa marehemu alikuwa kaolewa na bwana mzungu aliyeitwa  Andrew Harvey. Kwa maelezo ya Andrew yalikuwa makubaliano yake na mkewe kuwa ndoa yao iwe siri. Harvey pia alisema alikwisha mtaarifu Prezzo kuwa waliyoyafanya BBA ilikuwa kama filamu hivyo aache kutangaza ndoa na binti huyo.
Harvey amerudia tena baada ya msiba kumtaarifu Prezzo aache kuiongeza machungu familia yake kwa maneno yake kuwa ataelekea Nigeria kwenye msiba wa mchumba wake. Wakati huo huo habari zimeanza kuenea kuwa kifo cha Goldie kimetokana na matumizi ya madawa ya kulevya, kadri ya watu waliokuwa karibu sana na marehemu. Kadri ya habari hizo Goldie tayari alikuwa kesha wahi kupata matatizo kutokana na matumizi ya madawa hayo, na safari hii matatizo yalisababisha kifo chake.
Mungu amrehemu amuweke pema peponi