Skip to main content

Posts

Showing posts from September 18, 2011

Mahafali ya 6 ya THT ilikuwa tamu sana

Jana nilihudhuria mahafali ya 6 ya THT.Kilikuwa ni kitu kizuri sana, kama mwanamuziki nilipata faraja sana kuona vijana wakiwa wamefuzu na kuwa na taaluma ya uimbaji ya hali ya juu. Kila mtu mwenye mdomo kwa ujumla anaweza kuimba, lakini kuweza kuimba kwa hisia mpaka anaekusikiliza akapata hisia ndiyo inayotofautisha waimbaji na wapiga kelele. Jana nilibahatika kusikia waimbaji tena wengi.. Pia katika mahafali yale palitolewa maelezo kuwa kuna kituo kingine kule Temeke ambako kuna fanyika shughuli kama hiyo ambapo pia alipanda kijana mdogo kutoka huko na kuweza kuimba vizuri mno kuongeza furaha yangu. Jambo lililokuwa wazi kitaaluma staili ya uimbaji wa yule kijana wa Temeke ilikuwa tofauti na hawa waliofuzu toka THT, jambo ambalo linatoa funzo kuwa kuna hitajika vituo zaidi ili kuweza kutoa aina mbalimbali za uimbaji. Funzo jingine ni kuwa una hitajika vituo vya kufundisha ala za muziki na upigaji. Hii inadhihirika hata katika nyimbo mbalimbali zinazorekodiwa siku hizi. Taaluma ya upa…