Mahafali ya 6 ya THT ilikuwa tamu sana



Abdul Salvador, Waziri Ally na King Kiki

Mmoja wa waalimu Cardinal Gento hongera kwako.

Waziri Ally na Karola Kinasha




Jana nilihudhuria mahafali ya 6 ya THT.  Kilikuwa ni kitu kizuri sana, kama mwanamuziki nilipata faraja sana kuona vijana wakiwa wamefuzu na kuwa na taaluma ya uimbaji ya hali ya juu. Kila mtu mwenye mdomo kwa ujumla anaweza kuimba, lakini kuweza kuimba kwa hisia mpaka anaekusikiliza akapata hisia ndiyo inayotofautisha waimbaji na wapiga kelele. Jana nilibahatika kusikia waimbaji tena wengi.. Pia katika mahafali yale palitolewa maelezo kuwa kuna kituo kingine kule Temeke ambako kuna fanyika shughuli kama hiyo ambapo pia alipanda kijana mdogo kutoka huko na kuweza kuimba vizuri mno kuongeza furaha yangu. Jambo lililokuwa wazi kitaaluma staili ya uimbaji wa yule kijana wa Temeke ilikuwa tofauti na hawa waliofuzu toka THT, jambo ambalo linatoa funzo kuwa kuna hitajika vituo zaidi ili kuweza kutoa aina mbalimbali za uimbaji.
Funzo jingine ni kuwa una hitajika vituo vya kufundisha ala za muziki na upigaji. Hii inadhihirika hata katika nyimbo mbalimbali zinazorekodiwa siku hizi. Taaluma ya upangaji wa vyombo (arrangement) bado iko chini. Faraja nyingine ilikuwa ni kuwepo kwa wanamuziki wa zamani ambao wote nilioongea nao hawakuwa na jingine zaidi ya sifa kwa kituo hiki. Hongera THT Picha kwa hisani ya www.michuzijr.blogspot.com

Comments