Wednesday, November 5, 2014

FILAMU YA KUTAKAPOKUCHA JOHN KITIME NA MZEE MAGALI NDANI

ILE  muvi ambayo mwanamuziki John Kitime alishiriki akiwa na wasanii wengine wakongwe akiwemo mzee Magali na waalimu mahiri wa sanaa kutoka TASUBA, hatimae itakuwa dukani 24 november 2014, ikisambazwa na kampuni ya Proin Promotions Ltd. Filamu hii ilikuwa iwe dukani mwezi June lakini ikasubirishwa ili kufanyiwa editing zaidi.Katika filamu hii, John Kitime ni Mwenyekiti wa kijiji anaejiona Nusu Mungu na hasa pale ambapo mwanae , ambae ni mpiga karate mashuhuri anapoingia Kijijini na kutisha watu kwa kupiga watu hovyo hapo Kijijini. Mzee magali na mwanakijiji ambaye amepata elimu na anaweza kuzungumza Kiingereza jambo ambalo mwenyekiti wa Kijiji anaona ni tatizo kwani anaweza kunyang'anywa uongozi na msomi huyu. Ni picha yenye vituko, vichekesho, na muziki unaopigwa na gitaa na yeye Kitime. Hadithi imeandikwa na Irene Sanga. Angalia picha za utengenezaji wa muvi hii.
KARIBU INTERNATIONAL MUSIC FESTIVAL NOV 7-9 2014 BAGAMOYO


Tamasha kubwa la Karibu International Music Festival, litafanyika katika viwanja vya TASUBA Bagamoyo kuanzia Novemba 7-9 Mwaka huu wa 2014.

Vikundi zaidi ya 30 na wasanii zaidi ya 500 kutoka kila kona ya dunia wanataraji kushiriki.

“Lengo kuu la Tamasha, pamoja kukazia katika kurasimisha tasnia ya muziki kuwa na umakini zaidi, lakini kingine ni kukuza uchumi wa eneo husika la Bagamoyo ambalo ni la kihistoria, pamoja na kuhakikisha sanaa ya asili ya mtanzania inapata kuonekana katika jukwaa la kimataifa,”alisema Lupia.

Katika tamasha hili kila kitu kitakuwa ‘live’ hakutakuwa na playback Pia kutakuweko na warsha mbalimbali kwa ajili ya wanamuziki na wadau watakao hudhuria.