Skip to main content

Posts

Showing posts from May 21, 2012

Robin Gibb wa BeeGees afariki dunia kwa kansa ya tumbo

Robin Hugh Gibb, mwanamuziki wa kundi maarufu la BEE GEES amefariki. Robin  alizaliwa tarehe  22 Desemba mwaka 1949.  Kundi la Bee Gees lilianzishwa kwa pamoja na pacha wake Maurice na kaka yao Barry japo Robin ndie aliyejulikana zaidi katika kundi hili. Wazazi wao walikuwa Waingereza japo kwa kipindi fulani walihamia Australia. Inasemekana kundi hili ndilo lililokuwa na mafanikio kuliko kundi lolote jingine la Pop duniani. Kwa karibu miongo 6 kundi hili limekuwa jukwaani. Kundi liliweza kuuza zaidi ya santuri milioni 200.
 Watanzania wengi walianza kuwafahamu baada ya kusikia vibao vyao kama Staying Alive, Night Fever, How deep is your love na kadhalika  katika filamu ya filamu ya Saturday Night Fever. 
Tarehe 20 May 2012 Robin amefariki baada ya matatizo ya muda mrefu ya kansa ya utumbo. Pacha wake Maurice alifariki kwa tatizo hilohilo 2003.
Grammy Awards za BeeGees
1977 Best Performance by a Group — "How Deep Is Your Love" 1978 Best Performance by a Group — "Night Fev…