Sunday, May 1, 2011

Week-end ya MoshiMoshi mji ulioko chini ya mlima mrefu kuliko yote Afrika, ni mji unaochemka wiki-endi ikifika. Kimuziki kuna bendi kadhaa ambazo huwa jukwaani kwenye sehemu mbalimbali za mji huu. Week-end ya tarehe 30 April 2011, ilinikuta Moshi baada ya shughuli ya siku ya wazazi kwenye shule ya binti yangu. Hivyo jioni wenyeji wa Moshi akiwemo Louie Kifanga na mtangazaji maarufu wa Moshi FM Mtoli Mayombola, walihakikisha napitia baadhi ya sehemu zilizo na muziki. Moshi kuna bendi zifuatazao Dozee Musica, Kuringe Sound, Family Musica,Today band, Moshi Police Jazz Band. Nilipata bahati ya kushiriki na Family Musica wakiwa katika ukumbi wa saria Road House. Mambo yalikuwa rahaaaaaa kwa sanaaa
Ignas Ngalye Solo Gitaa na Muimbaji

Henry Masala Drums, Bass, Muimbaji

David Ngalye, Bass, Keyboards na Muimbaji

John Kitime na Mtoli Mayombola wa Moshi FM