Wednesday, February 29, 2012

Shaaban Lendy arudi Msondo

Shaaban Dede ambaye nae amewahi kuhama kutoka Sikinde na kwenda Msondo mara kadhaa,Katikati ni Ally Jamwaka, kulia mwisho ni Shaaban Lendy

Mpiga saxaphone mkongwe Shaaban Lendy amerudi tena katika kundi la Msondo Group ambalo aliwahi kuweko miaka ya nyuma. Msondo wamekuwa kwa muda mrefu wakiwa na wapiga trumpet tu, tofauti na mfumo wa miaka mingi wa Msondo ambapo kulikuwa na Tenor Sax, Alto Sax na trumpet kadhaa. Sasa tutaweza kusikia tena utamu wa mchanganyiko wa Sax na trumpet katika nyimbo za Msondo

Dar Live kuleta Hip Hop Night


Extra Bongo Band yajitoa katika kinyang'anyiro cha Kili Music Awards

Kiongozi Mkuu wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choky ametangaza kuwa bendi yake haitashiriki katika sekeseke la kutafuta tuzo la Kili Music Awards. Katika kuelezea sababu za hatua hiyo , Choky alisema sababu kadhaa zimepelekea hayo. Kwanza ni kuwa bendi yake tangu mwaka jana ilikwisha andika barua ya kutotaka kushirikishwa katika mtiti huo. Sababu nyingine ni ule muundo wa kundi ambalo linaitwa 'Wimbo Bora wa Kiswahili (Bendi)'. Kiongozi huyo alisema kundi hili limedharauliwa kwani katika makundi mengine kuna waimbaji bora wa kike na wakiume wa kundi na kutokana na bendi kuweko za aina nyingi kundi hili limebanwa kuonyesha kuwa linadharauliwa na watayarishaji. Wengine waliokuwemo katika kundi hili ni African Stars- Dunia Daraja, Mashujaa Band-Hukumu ya Mnafiki, Mapacha Watatu -Usia wa Babu,Extra Bongo walikuwa na nyimbo mbili katika kundi hili Falsafa ya Mapenzi na Mtenda.Kwa kupiga kura Kili Music Award bonya HAPA
Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...