Extra Bongo Band yajitoa katika kinyang'anyiro cha Kili Music Awards

Kiongozi Mkuu wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choky ametangaza kuwa bendi yake haitashiriki katika sekeseke la kutafuta tuzo la Kili Music Awards. Katika kuelezea sababu za hatua hiyo , Choky alisema sababu kadhaa zimepelekea hayo. Kwanza ni kuwa bendi yake tangu mwaka jana ilikwisha andika barua ya kutotaka kushirikishwa katika mtiti huo. Sababu nyingine ni ule muundo wa kundi ambalo linaitwa 'Wimbo Bora wa Kiswahili (Bendi)'. Kiongozi huyo alisema kundi hili limedharauliwa kwani katika makundi mengine kuna waimbaji bora wa kike na wakiume wa kundi na kutokana na bendi kuweko za aina nyingi kundi hili limebanwa kuonyesha kuwa linadharauliwa na watayarishaji. Wengine waliokuwemo katika kundi hili ni African Stars- Dunia Daraja, Mashujaa Band-Hukumu ya Mnafiki, Mapacha Watatu -Usia wa Babu,Extra Bongo walikuwa na nyimbo mbili katika kundi hili Falsafa ya Mapenzi na Mtenda.Kwa kupiga kura Kili Music Award bonya HAPA












Comments