Sunday, March 18, 2012

Umeme ulikatwa saa 8 usiku,katikati ya dansi la Njenje, lakini watu walisubiri mpaka uliporudi saa 9 na kuendeleza raha

Pamoja na TANESCO kuondoa umeme katikati ya maraha ya dansi, kiasi cha saa 8 na robo usiku, wapenzi wa muziki katika ukumbi wa Salender Bridge hawakuondoka mpaka uliporudi karibu saa nzima baadae. Na burudani iliendelea kwa msanii Anania Ngoliga kupanda jukwaani kisha Kilimanjaro Band ambao ndio walikuwa wenyeji na hatimae East African Melody ambao walimaliza raha ya usiku huo na kuwaacha wapenzi wakiwa bado wana kiu cha kuendeleza starehe.

Rebecca Malope kuwepo katika Tamasha la Muziki wa Injili


Rebecca Malope kuwepo katika Tamasha la Muziki wa Injili April 8 2012 Uwanja wa Taifa. Muimbaji huyu mahiri kutoka Afrika Ya Kusini  ana historia ya muziki inayoanzia 1986. Wakati huo Rebecca akiwa na umri wa miaka 21 na akiwa na dada yake Cynthia waliondoka kwao Lekazi na kusafiri kwa shida hadi mji wa Evaton kiasi cha kilomita 400 na baadae kuingia jiji la Johannesburg wakiwa na nia moja tu kuwa wanamuziki. Rebecca amekwisha toa album 32 na pia kupata tuzo ya Kora kwa muziki wa Gospel.