Skip to main content

Posts

Showing posts from April 21, 2013

RUSHWA KWENYE MUZIKI

RUSHWA ni mdudu anayesumbua sana jamii ya Tanzania. Kwa mtazamo wangu, rushwa inakuwa ngumu kupiga vita zikiwemo sababu kadha wa kadha, kwa mfano, kuna watu ambao kwao rushwa wala si kosa bali ni taratibu za kawaida za maisha, mtu ambaye alimuona baba yake maisha yake yote tangu mtoto, akitoa rushwa na mambo yakawa yanaenda vizuri sana, pengine hata vyeti vyake vya shule na hata kazi anayofanya ilitokana na baba yake kutoa rushwa na yeye analijua hilo, na amefanikiwa, mtu kama huyu rushwa ndio utaratibu bora wa maisha yenye mafanikio, kamwe hataipiga vita. Kuna wengine ambao si wala rushwa lakini rafiki zao na ndugu zao ni wala rushwa, na wanaishi vizuri kutokana na mapato ya rushwa kamwe hawawezi kupiga vita rushwa. Kuna wale ambao ni wengi, ambao wakijaribu kutoa taarifa kuhusu rushwa maisha yao yatakuwa magumu, kwa mfano, mtu huyu akienda kulipa kodi kwa njia ya rushwa analipa robo ya bei ambayo angelipa kama angelipa kihalali, huyu kamwe hatapiga vita rushwa. Kuna wale ambao wanao…