Thursday, July 14, 2011

The Talent Band

Kama kawaida yangu nilikuwa kwenye mizunguko masikio yakisikiliza sauti yoyote itakayoonyesha kuna muziki mahala, nilizunguka Ilala nikakuta kuna tatizo la mgao wa umeme, sehemu kubwa ni giza nikasikia muziki, kumbe ni Jahazi Modern Taarab wanapiga lakini wakitumia jenereta. Ikawa ngumu kuingia muziki huo kwani usalama ulikuwa mchache nje ya ukumbi. Nikaelekea Manzese na huko nikasikia muziki. Kusogea kumbe ni mwanamuziki wa zamani Hussein jumbe akiwa na kundi lake la Talent Band. Nilimkuta akipiga kibao cha Msondo Ngoma ni raha kama kawaida.


Mkono wa Chuma

Simba Lion

Mapambo

Hamis Buyugwa

George Mbata

Hussein Jumbe
IVORY BAND YAPANIA KUPAA KATIKA ANGA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA

Ijumaa hii na kila Ijumaa ni siku ya raha na starehe kwa wakazi wa Tabata na vitongoji vyake, maana mara tu baada ya jua kuzama kiota maaru...