Skip to main content

Posts

Showing posts from June 2, 2012

Elimu ya sanaa irudishwe tena mashuleni kuanzia shule za awali

Asilimia kubwa ya wanamuziki hapa Tanzania wanapiga muziki bila ya kuwa na elimu yoyote ya awali ya muziki. Viongozi wengi wa nchi wamekuwa wakitoa kauli nzuri za kusifu sanaa hii na wasanii wa sanaa hii lakini ni nadra kusikia kiongozi akiongelea matayarisho rasmi katika sanaa hii, na kwa ukweli hata katika sanaa nyingine. Kama ambavyo kumekuweko na kufa kwa viwanda nchini humu ndivyo ilivyotokea katika elimu ya sanaa. Zamani sanaa ilianza kufundishwa kuanzia darasa la kwanza, na hata syllabus ya elimu hiyo mpaka leo ipo, ila haitumiki. Vyuo, kama Chuo cha Waalimu Butimba kule Mwanza, kilitoa waalimu ambao walikuwa maalumu kwa ajili ya kufundisha sanaa katika shule zetu kuanzia shule za msingi, bahati mbaya sana haya yote yametupwa uvunguni, hivyo Taifa linakwenda kihobelahobela katika tasnia ya sanaa. Kuna vyuo, kwa mfano Chuo cha Sanaa Bagamoyo, ambacho hupokea wanafunzi kwa ajili ya kupata elimu ya sanaa, lakini utaona wazi kwa kuwa hakuna mtiririko wa elimu hiyo kutokea shule za m…