Skip to main content

Posts

Showing posts from September 9, 2016

MUZIKI NI BURUDANI, LAKINI BURUDANI KWA NANI?

Pombe ni burudani kwa mnywaji, lakini si burudani kwa mtengeneza pombe. Pale mtengeneza pombe atakapoanza kuburudika na pombe yake mwenyewe, ndio utakuwa mwisho wa yeye kufaidika kiuchumi na pombe hiyo. Hali kadhalika katika muziki burudani ni kwa wasikilizaji, na pale mwanamuziki anapotekwa na muziki wake kuwa burudani kwake, swala la muziki huo kumpa faida za kiuchumi hupungua. Kwa miaka mingi muziki katika nchi yetu umekuwa ukisisitizwa kuwa ni burudani, jamii huitaja hivyo vyombo vya habari husisitiza hivyo, japo vingine huingiza mabilioni ya shilingi kwa mwaka kutokana na ‘burudani’ hiyo. Kutokana na mambo kadhaa, ni wazi kuwa serikali pia huamini muziki ni burudani tu. Utamaduni huu ni moja ya sababu kubwa kwanini wanamuziki wa Tanzania hawafaidi matunda ya kazi yao kama wanavyofaidi wenzao wa nchi nyingine, japo mara nyingine ubora wa muziki wa Tanzania ni sawa na mara nyingine ni bora kuliko wa nchi nyingine. Juzi juzi nilipata bahati ya kuongea na mama mmoja ambaye alikuwa mm…