Skip to main content

Posts

Showing posts from September 11, 2012

IJUE HISTORIA YA KHADIJA MNOGA-KIMOBITEL

Khadija Mnoga alizaliwa Dar es Salaam maeneo ya Mwananyamala, na kuanza elimu ya msingi Shule ya Mwongozo iliyoko Kinondoni ambako alimaliza 1995, kisha akajiunga na shule ya sekondari Navy Kigamboni. Alipokuwa shuleni alikuwa mpenzi sana wa michezo na wala hakuwa na muonekano wowote wa  kipaji cha muziki. Lakini mwanzoni mwishoni mwa miaka ya 90 akajiunga na kikundi cha CCM cha Chipukizi Mwananyamala ambapo walianzisha kwaya na hapo ndipo kwa mara ya kwanza alijijua anauwezo wa kuimba alipoona watu wanaanza kumsifu. Diwani mmoja wa wakati huo, marehemu Ndege alikinunulia kikundi chake yunifomu na kikawa kikundi rasmi kwenye mikutano yako na ni toka wakati huo akaanza kufaidi kutuzwa  na hata ikafikia anatuzwa laki nzima katika onyesho. Wenzie katika vikundi hivyo vya chipukizi ndio walioanza kupandikiza mbegu ya kuanza kutamani kuimba kwenye jukwaa kubwa, hata Khadija mwenyewe akaenda kumwambia mama yake kuwa anajiona anauwezo wa kuimba kwenye bendi, mama yake hakumuunga mkono lakin…