Wednesday, November 28, 2012

BURIANI SHARO MILIONEA

MAMIA YA WASANII NA WANANCHI WENGINE WALISHIRIKI KATIKA MAZISHI YA MSANII ALIYETOKEA KUPENDWA SANA KIPINDI CHA KARIBUNI KUTOKANA NA KUWA MAHIRI KATIKA AINA YAKE YA MUZIKI NA AINA YAKE YA UCHEKESHAJI, SHAROMILIONEA. MAZISHI YALIFANYIKA MUHEZA TANGA KIJIJI KWAO MAREHEMU. MWENYEZI MUNGU MWENYE REHEMA AMLAZE PEMA PEPONI AMINA
 KWA PICHA ZA MAZISHI HAYO BONYEZA hapa

KUHUSU RAYC

Kuna watu wengi wamekuwa wakiuliza kuhusu hali ya RayC, kuna mtu ambaye kwa sababu ambazo hazijulikana aliaanza kuzusha taarifa ya kifo cha RayC jana mchana, blog hii ilipigiwa simu kadhaa ambazo zimeendelea mpaka leo kuulizia ukweli kuhusu taarifa hiyo. TAARIFA HIYO NI UWONGO MTUPU. Moja ya watu walioweka kwenye ukurasa wake wa Facebook taarifa hii ni mwanafunzi aliyeko Urusi aitwaye Musa, na alipojaribu kuhojiwa kuhusu hilo aliishia kujibu kwa matusi. Katika wiki hii ya majonzi katika tasnia ya sanaa pia msanii mwingine alizushiwa kifo na kulazimisha blog hii kuwasiliana na viongozi wa tasnia ya msanii husika kuulizia kuhusu hili, pia hilo lilikuja julikana kuwa ni uwongo. Swali ni mtu wa namna gani unaweza kuzua kuwa binadamu mwenzio amefariki wakati unajua ni uwongo mtupu? Miezi kadhaa iliyopita blog hii ilitumiwa sms , tena na mwandishi mwenye heshima kuwa mwanamuziki fulani aliyekua nje ya nchi amefariki na kuwa eti amezikwa Magomeni tayari, ililazimika kumpigia simu mwanamuziki mwenyewe ambaye bahati nzuri alipokea simu mwenyewe akiwa mzima wa afya. Chonde ndugu zangu tabia hii chafu lazima ikome.
Hapa nawaunganisha kusikia sauti ya mama yake RayC akiongea kuhusu uzushi huo


Sauti kwa hisani ya www.millardayo.com

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...