Skip to main content

Posts

Showing posts from August 14, 2012

Alphabeta Music Centre

Mark Manji amekuwa mpenzi wa muziki katika maisha yake yote na baada ya kustaafu kazi akaona ni heri afanya kile kitu ambacho amekuwa akikipenda katika maisha yake yote nacho ni muziki. Lakini si kwa kupiga muziki maana alishwa wahi kupiga muziki katika ujana wake, na hata kuwa na bendi na akajikuta akiangushwa na matukio. Aliwahi kununua vyombo vya bendi kutoka kwa Marealle wa Seview na kupiga muziki kwa muda mfupi, lakini akawa amepata kazi nje ya nchi akamrudishia tena vifaa hivyo bwana Marealle, baadae alipopata nafasi ya kununua vyombo akawa ananunua vichache vichache na hatimae kuwa na vifaa vya kutosha bendi. Karama Malegesu na vijana wenzie waliweza kumshawishi Manji kuanzisha bendi naye akaiita Chikoike Sound(jina lililotokana na kuunganisha majina ya wanawe), bendi ilianza 1994, kati ya wanamuziki waliopitia bendi hiyo ni waimbaji Banza stone na Juma Malembeka. Kwenye mwaka 1999 baadhi ya wanamuziki wakamuibia vyombo vyake fulani, akaamua kufungia vyombo vyake, na hatimae b…