Mark Manji amekuwa mpenzi wa muziki katika maisha yake yote na
baada ya kustaafu kazi akaona ni heri afanya kile kitu ambacho amekuwa
akikipenda katika maisha yake yote nacho ni muziki. Lakini si kwa kupiga muziki maana
alishwa wahi kupiga muziki katika ujana wake, na hata kuwa na bendi na akajikuta akiangushwa na matukio. Aliwahi
kununua vyombo vya bendi kutoka kwa Marealle wa Seview na kupiga muziki kwa
muda mfupi, lakini akawa amepata kazi nje ya nchi akamrudishia tena vifaa hivyo bwana Marealle, baadae alipopata nafasi ya kununua vyombo akawa ananunua vichache vichache na hatimae kuwa na vifaa vya kutosha bendi. Karama Malegesu na vijana wenzie waliweza kumshawishi Manji kuanzisha bendi naye akaiita Chikoike Sound(jina lililotokana na kuunganisha majina ya wanawe), bendi
ilianza 1994, kati ya wanamuziki waliopitia bendi hiyo ni waimbaji Banza stone na Juma Malembeka. Kwenye mwaka 1999 baadhi ya wanamuziki wakamuibia vyombo
vyake fulani, akaamua kufungia vyombo vyake, na hatimae baada ya kustaafu
akaamua kufungua kituo cha kufundishia muziki.
Mark Manji |
Kituo hiki kiko Tabata Liwiti karibu kabisa na kituo cha
posta Tabata. Kituo hiki ambacho
kina waalimu wenye uzoefu wa miaka mingi hakina wanafunzi wengi hivyo kila
mwanafunzi kupata nafasi ya kufundishwa vema, kina vifaa bora vya kisasa na pia
kuna studio nzuri ya kurekodi iliyoko katika maeneo ya kituo.
Comments