Skip to main content

Posts

Showing posts from April 27, 2012

Muziki wa Dansi umezidiwa ujanja na Taarab?

Wakati wa Top Ten Show, onyesho lililokuwa kubwa sana la mashindano ya bendi, ambapo bendi kutoka mikoa yote zilipata nafasi sawa za kuonyesha uwezo wao na hatimae kuchaguliwa Bendi Bora, vikundi vya muziki wa Taarabu havikushirikishwa  kwa kuwa vilikuwa vikipiga muziki tofauti na bendi za muziki wa dansi, palikuweko hata malalamiko kutoka kwa baadhi ya bendi ya kupinga kundi la Varda Arts ambalo lilikuwa likipiga muziki wake kufuatia mirindimo ya Kihindi kushiriki katika shindano hili. Hata vyama vya muziki wa Taarab na muziki wa dansi vilikuwa tofauti. CHAMUDATA (Chama  cha Muziki wa Dansi Tanzania) kwa ajili ya muziki wa ‘dansi’ na TTA (Tanzania Taarab Association) kwa ajili ya muziki wa Taarab. Mambo yamebadilika sana siku hizi, sioni hata sababu ya kuwa na vyama viwili kwa  kuwa tofauti  za kimuziki za makundi haya zimepotea sana
 Kila nikiingia  katika kumbi mbalimbali kuangalia na kuburudika na kazi kutoka  vikundi vinavyojitambulisha kuwa ni vya Taarab na vile vinavyojitambulis…