Friday, May 27, 2011

Cassava Band

Nilikuwa napita karibu na Maryland Bar Mwenge, nikasikia wimbo Kadiri kansimba ukipigwa na kuimbwa vizuri, sikuwa na ujanja ilikuwa lazima nikaione bendi inayopiga vizuri namna hiyo, nilipata mshangao. Nusu ya wanamuziki nawafahamu na sijaonana nao siku nyingi. Kwenye drum alikuweko Kejeli Mfaume, huyu tulikuwa nae Tancut Almasi na ndie aliyerekodi nyimbo nyingi za awamu ya kwanza ya Tancut Alimasi na sasa alikuwa pia anaimba kwa sauti tamu, kweli miaka inapita Kejeli hakuwa anaimba enzi hizo. Mshangao wa pili ni kumwona Sakul kwenye solo, mara ya mwisho nilimkuta Sakul Tabora Hotel akiwa na bendi moja huko, Sakul ana ulemavu wa macho haoni lakini kwenye solo wacha kabisa. Pembeni yake kwenye gitaa la rythm alikuweko Kienze, huyu nilifahamiana nae mara ya kwanza mwaka 1995, wakati huo akiwa katika kundi la SBB- Seven Blind Beats, nae pia ana ulemavu wa macho haoni, lakini kwa rythm gitaa kaa mbali. Wakali hawa watatu wakiwa pamoja lazima kieleweke. Nikajikuta nachukua gitaa na tukapiga Masafa Marefu, tukapiga Mtaulage loh nilirudishwa mbaali. Thanks guys

Kejeli Mfaume

Kienze-Rythm Gitaa

Sakul-Solo gitaa


Ally


Ally Konde

Juma
Ngoma MusicaNilikuwa napita maeneo ya Sinza Makaburini nikasikia muziki toka kwenye bar moja, kuingia hapo nikakuta bendi yenye vyombo saafi ikikandamiza sebene na kutoa show ya nguvu si wengine ni Ngoma Musica

Kings Modern Taarab

 Leo nilikaribishwa kwenye kikao cha kundi jipya la Taarab, Kings Modern Taarab, Jina hilo linatokana na mahala wanapofanyia mazoezi, Kings bar Mburahati. Kundi hilo lenye wasanii 18, liko chini ya Kijoka, mtunzi na muimbaji wa siku nyingi. Tayari wamekwisha rekodi album mbili ambazo hawajazizindua na hivyo walikuwa katika vikao vya kupanga ratiba za uzinduzi. Nyimbo ambazo tayari ziko redioni ni Mchumia juani, na zilizo katika video kwenye TV ni Roho Mbaya, Masharoharo, na nyingine mbili


Kijoka

Sakama live Show Band jukwaani leo Brighton


Kwa wale wa Uingereza .............Kundi zima la Sakama live Show Band leo litakuweko katika  ukumbi wa  The Komedia, Brighton UK, Kuanzia Saa 1.30 na nusu usiku (7.30 pm), kiingilio ni  £10/£12, kukosa ni kosa. Njoo uinjoy music na kukutana na marafikiHaya wasanii chipukizi jitokezeni mtumie nafasi hii

Wanamuziki wengi maarufu duniani wametokana na kupatikana katika maonyesho au mashindano ya aina kama hii.Nashauri wanaoweza kujitokeza wajitokeze tuwaone.
Fomu za kuwapata washiriki watakaounda kundi la muziki wa Bongo Fleva kupitia Shindano la Jenga Nchi Yako, zimeanza kutolewa katika Ofisi za Kampuni ya Global Publishers Bamaga-Mwenge, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mratibu wa shindano hilo, Richard Manyota(Pichani), mchakato ulianza wiki hii kwa kila mshiriki kujipatia fomu hiyo kwa shilingi 3,000, walengwa wakiwa ni wakazi wa Jiji la Dar es Salaam pekee na wasanii watakaofanikiwa kuunda kundi hilo watarekodi wimbo mmoja bure.

Mratibu huyo aliwataka wakazi wa Dar es Salaam na vitongoji vyake wajitokeze kwa wingi kuchukua fomu hizo kwa sababu zilizopo ni chache.

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...