Skip to main content

Posts

Showing posts from April 7, 2013

SURPRISE YA MWAKA......BABA YAKE NYOTA NDOGO ALIKUWA MWANAMUZIKI MTANZANIA

-->


Nyota Ndogo  ni jina maarufu sana Afrika Mashariki, ni mwanadada mwanamuziki mwenye sauti tamu sana, kati ya vibao vyake vyote nikiri kuwa wimbo wake wa Watu na Viatu ambao ulishinda tuzo katika Tanzania Music Awards 2007, niliupenda sana, pia huyu binti ambaye amekwisha toa album kadhaa zikiwemo Chereko, Nimetoka Mbali na Mpenzi, alizaliwa 1981 na akapewa jina la Mwanaisha Abdallah.
Mwanaisha alizaliwa Mombasa  hakumaliza shule na katika kazi alizopitia ni pamoja na msaidizi wa nyumbani. Katika kuonyesha tena kuwa wanamuziki wengine muziki umo kwenye damu, baba wa binti huyu alikuwa mwanamuziki. Katika maelezo ya rasmi ya Nyota Ndogo baba yake alikuwa mwanamuziki wa bendi moja wapo Mombasa na aliitwa Abdallah Hatibu.  Blog ya www.wanamuzikiwatanzania.blogspot.com ambayo ni maarufu kwa kutafiti historia ya wanamuziki wa zamamni wa hapa nchini iliweka historia fupi ya kundi maarufu la Jamhuri Jazz Band, pamoja na picha ya mmoja wa wanamuziki wa bendi hiyo aliyeitwa Abdalla…