Saturday, February 15, 2014

MTANDAO WA WANAMUZIKI TANZANIA WAPATA OFISI MPYA

Baada ya kuwa na ofisi ya muda ambayo ilikuwa katika mazingira magumu kikazi hatimae Mtandao wa Muziki Tanzania umepata ofisi mpya yenye hadhi ya kuitwa ofisi ya wanamuziki. Ofisi hiyo iko katika barabara inayoelekea Mahakama ya Kinondoni, katika jengo la ghorofa lililojengwa kwa matofari ya kuchomwa. Ofisi iko ghorofa ya 3 chumba na 148. Wanamuziki mnakaribishwa kuitumia ofisi hiyo

AFRICAN STARS WALIKUWA MZALENDO PUB CHUNGULIA HAPAAKUDO NA MAPACHA WATATU NAO VALENTINE

Jana ilikuwa siku ya Valentine, kumbi mbalimbali zilikuwa na maraha ya aina mbalimbali niliweza kuonja raha hizo. Letasi Pub pale Victoria Mapacha Watatu na ndugu zao Akudo Band waliliporomosha rumba usiku kucha,
AKUDO HAOOOOO

MAPACHA WATATUYALIYOJIRI ESCAPE ONE JANA


Jana ilikuwa Valentine, kumbi mbalimbali zilikuwa na maraha ya aina mbalimbali niliweza kuonja raha hizo. Escape One Mlalakuwa kulikuwa na Odama band, Juma Kakere na bendi yake, binti mdogo mwenye sauti tamu, Kadija, Linex na Kilimanjaro Band, baada ya hapo likafuatia disco la muziki wa zamani kidogo mpaka alfajiri. Letasi Pub pale Victoria Mapacha Watatu na ndugu zao Akudo Band waliliporomosha rumba usiku kucha, jirani hapo Mzalendo Pub, African Stars wana Twanga Pepeta walikuwapo. Kiukweli siku ya wapendanao kwa eneo hili ilifana sana.
MAMBO YA ESCAPE ONE
ODAMA BANDWATANGAZAJI WA RADIO CLOUDS WALIAMUA KUPANDA JUKWAANI NA KUIMBA, SITAKI KUSEMA KITU, ALIYEKOSA UTAMU KAKOSA


JUMA KAKERE NA BENDI YAKE

WANANJENJE---NYOTA YULEEEEE AKIFANYA MAMBO YAKE KAMA KAWAIDA