Saturday, September 15, 2012

A NEW BAND IN TOWN -SKYLIGHT BANDKuna bendi mpya mjini inaitwa SKYLIGHT BAND, bendi ya vijana ambayo jana nilipata nafasi ya kuonja muziki wao. Nilikuwa mtu wa mwisho kuondoka ukumbini jambo ambalo ni nadra kutokea kwangu, naweza kufanya hivyo kwa bendi ambayo imenifurahisha mpaka ninalazimika kukaa hadi mwisho. Watchout for this band wakikaa mwaka mmoja na seriousness waliyonayo sasa ni wazi Tanzania tutakuwa na bendi nyingine ambayo itaweza kusikika nje ya mipaka ya nchi yetu

HONGERA MISS UTALII-ILALA/KINONDONI
Jioni ya jana ilinikuta nikizunguka sehemu mbalimbali zilizokuwa na burudani. Niliamua kuanza safari zangu kwenye shughuli ya kumtafuta  Miss Utalii wa Ilala na Kinondoni, shughuli ilifanyika Hotel Lamada Msimbazi. Nilipofika mahala pa kukatia tiketi nikakuta jamaa 'wanapiga panga’,'wanachakachua', ukiwapa fedha za kiingilio wanakuamrisha uingie ndani bila kukata tiketi, nikang’ang’ania kupewa tiketi yangu tukaanza kuzungushana, nikaanza kuulizwa maswali kama nina complementary ticket’, nikawaambia, 'Jamani si nimewalipa alfu kumi naomba tiketi', ‘We mzee ingia tu’, nilijua mtayarishaji yuko bize huko akijua kuna watu mlangoni kumbe hakuna kitu, hatimae akaja jamaa mwenye headphone kama bodyguard akalazimisha nipewe tiketi ikachanwa nikaingia. Japo katika dakika za mwanzo kulikuwa na ukimya ambao ulikuwa unaleta uvivu, MC alipoingia alianza kuupa uhai usiku wa Utalii. Kwa kweli niliweza kuona tofauti kubwa kati ya Miss Utalii na Miss Tanzania, nimeipenda zaidi Miss Utalii kwa kuwa ilikuwa imechangamka zaidi ukiachia kipengele cha wasichana kujitambulisha ambacho kilichukua muda mrefu sana ukikumbuka kuwa kulikuwa na washindani 26, na pia kule kuhangaika ku ‘cat walk’ ilikuwa ni vichekesho, watoto wa watu kuanza kutembea kama maroboti. Nilipenda  sana Uafrika uliokuwemo ndani ya onyesho hilo, muziki wa kiasili na uonyeshaji wa vipaji kwa kucheza ngoma za kiasili za Kitanzania. Baadae sikuelewa kwanini aliletwa ‘ Michael Jackson wa Tanzania aliyecheza Thriller fake, na baadae jamaa waliokuja kucheza Kwaito.  Jambo ambalo nategemea litakuwa somo zuri kwa watayarishaji wa Miss Utalii, ni kuwa wakati washiriki wakipita na kucheza ngoma za makabila mbalimbali, mabinti ambao kwa mtizamo wa kawaida wasingejihusisha na muziki wa kiasili, ndio walikuwa msitari wa mbele kucheza ngoma ya Kihaya, ngoma ya Kingoni, ngoma ya Kizaramo, na tena kuzicheza vizuri sana. Na hawa ndio walipiga kelele na kudharau Michael Jackson ‘fake’ alipomaliza kucheza. Kweli lilikuwa onyesho la Miss Utalii. Katika kipindi cha mwezi mmoja nimeangalia maonyesho mawili ya Mamiss ambayo yenye mlengo wa vipimo vya kizungu, na hili moja lenye vigezo vya kwetu, sina wasiwasi kuwa nilifurahishwa zaidi na Miss Utalii.

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...