Skip to main content

Posts

Showing posts from November 10, 2016

3 of 469 BODI YA FILAMU NCHINI YATOA MAFUNZO KWA WASANII WA FILAMU ZAIDI YA 300 MKOANI MWANZA

Katibu Tawala Msaidizi, kitengo cha elimu mkoani Mwanza, Khamis Maulid, akifungua warsha ya mafunzo ya filamu ya siku tatu mkoani Mwanza iliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini kwa ajili ya Wasanii wa Filamu mkoani Mwanza. Na BMG
Maulid amesisitiza wasanii hao kuhakikisha wanatengeneza filamu zenye ubora na zinazozingatia maadili ya mtanzania na kukaguliwa kabla ya kuingia sokoni hatua ambayo itasaidia kukuza soko la filamu mkoani Mwanza.
Pamoja na mambo mengine, warsha hiyo imelenga kuwawawezesha kielimu wasanii wa filamu mkoani Mwanza kutengeneza filamu zenye ubora, namna ya uanzishwa wa vikundi na kampuni za filamu, uandishi wa miswada ya filamu,uongozi wa filamu pamoja na taaluma ya upigaji picha. Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo, akielezea majukumu ya bodi hiyo ambayo ni pamoja na kuhakikisha ubora wa filamu pamoja na hakimiliki za wasanii wa filamu nchini. Wasanii wa filamu mkoani Mwanza wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo, wakati…