3 of 469 BODI YA FILAMU NCHINI YATOA MAFUNZO KWA WASANII WA FILAMU ZAIDI YA 300 MKOANI MWANZA

Katibu Tawala Msaidizi, kitengo cha elimu mkoani Mwanza, Khamis Maulid, akifungua warsha ya mafunzo ya filamu ya siku tatu mkoani Mwanza iliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini kwa ajili ya Wasanii wa Filamu mkoani Mwanza.
Na BMG

Maulid amesisitiza wasanii hao kuhakikisha wanatengeneza filamu zenye ubora na zinazozingatia maadili ya mtanzania na kukaguliwa kabla ya kuingia sokoni hatua ambayo itasaidia kukuza soko la filamu mkoani Mwanza.

Pamoja na mambo mengine, warsha hiyo imelenga kuwawawezesha kielimu wasanii wa filamu mkoani Mwanza kutengeneza filamu zenye ubora, namna ya uanzishwa wa vikundi na kampuni za filamu, uandishi wa miswada ya filamu,uongozi wa filamu pamoja na taaluma ya upigaji picha.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo, akielezea majukumu ya bodi hiyo ambayo ni pamoja na kuhakikisha ubora wa filamu pamoja na hakimiliki za wasanii wa filamu nchini.
Wasanii wa filamu mkoani Mwanza wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo, wakati wa warsha kwa wasanii hao hii leo.
Afisa Uendeshaji na Masoko kutoka Mfuko wa Pensheni PPF akielezea umuhimu wa wasanii wa filamu mkoani Mwanza kujiunga na mfuko huo ili kunufaika na mafao kutokana na kazi zao za sanaa. 

PPF ni miongoni mwa wadau waliosaidia kufanikisha warsha ya mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini.
Kutoka kushoto ni Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, Katibu Tawala Msaidizi, kitengo cha elimu mkoani Mwanza, Khamis Maulid pamoja na afisa  kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF.
Mjumbe wa Bodi ya Filamu Taifa kutoka mkoani Mwanza, Hussein Kimu (katikati) akiwa pamoja na wajumbe wengine wa bodi hiyo pamoja na wasanii wa Filamu mkoani Mwanza.
Zaidi ya wasanii 300 wa Filamu mkoani Mwanza wakifuatilia warsha ya mafunzo ya filamu yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini.
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, amesema mkoani Mwanza kuna fursa nyingi kwenye soko la filamu ikiwemo mandhari nzuri hiyo wasanii wa filamu mkoani Mwanza watumie fursa hiyo kuboresha soko lao la filamu.
Mjumbe wa Bodi ya Filamu Taifa kutoka mkoani Mwanza, Hussein Kimu, amesema mafunzo hayo yatawasaidia wasanii wa Filamu mkoani Mwanza katika kuboresha filamu zao na hivyo kuinua soko la Filamu mkoani Mwanza badala ya kutegemea soko hilo Jijini Dar es salam pekee.
Baadhi ya wasanii wa Filamu mkoani Mwanza wakipiga picha na viongozi Filamu nchini.
Mmoja wa wasanii wa Filamu mkoani Mwanza (kushoto) akisalimiana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo (katikati), kulia ni Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba.
Mmoja wa wasanii wa Filamu mkoani Mwanza (kushoto) akisalimiana na Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, katikati ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo
Viongozi mbalimbali, akiwemo Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba (wa kwanza kushoto), Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo (wa pili kushoto) pamoja na Innocent Mungy kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA (wa kwanza kulia).
Baadhi ya wasanii wa Filamu mkoani Mwanza wakipiga picha na viongozi Filamu nchini.

Comments