Friday, April 6, 2012

Steven Kanumba is no more, RIP Kanumba

Katika hali inayoleta mshangao na bumbuwazi, taarifa zilianza kuenea jijini Dar es salaam kiasi cha saa nane na nusu usiku kuwa Steven Kanumba amefariki. Habari ambazo zina uhakika ni kuwa maiti yake ilikuwa tayari imekwishapelekwa mochwari Muhimbili. Sababu ya kifo bado ni utata kwani kuna maelezo kuwa alianguka ghafla, kukiwa na maelezo mengine kuwa kulikuwa na ugomvi kwake.Pamoja na yote Mungu Amlaze Pema Kanumba, tulimpenda lakini Mungu amempenda zaidi.
Steven Kanumba died suddenly around midnight last night. His body is now lying at the Muhimbili Hospital Mortuary. The cause of death has been said was caused by a fight at his home . Rest In Peace Kanumba

Mbunifu wa amplifaya za Marshall aaga dunia

Kwa wapiga magitaa wengi duniani hasa wa muziki wa rumba na hata rock, hakuna amplifaya ilikuwa ikizidi ile ya aina ya Marshall. Amplifaya hizi zilikuwa na sauti bora, zilikuwa imara, na binafsi nilipendelea zaidi zile amplifaya zilizokuwa zinatumia valve kabla ya hizi za sasa zinazotumia IC, zilikuwa na aina ya pekee ya uzito wa sauti. Lakini ni jambo la kusikitisha mwanzilishi wa utengenezaji wa amplifaya hizi amefariki na kuacha urithi wa kazi yake dunia nzima. Mungu amlaze pema Jim Marshal aliyepewa jina "Father of loud'- Baba wa kelele kwa kuwa amplifaya zake zilikuwa maarufu sana kwa wanamuziki wakubwa wengi na zilitegemewa sana katika matamasha makubwa duniani. Soma hapa habari zake zaidi Jim Marshal