Skip to main content

Posts

Showing posts from September 28, 2011

Vituko vya baadhi ya wanamuziki wetu wakiwa nje ya nchi

Ni jambo la kusikitisha lakini kuna wanamuziki wengi wa Tanzania wamepoteza bahati ambazo si tu zingewaweka katika jukwaa la kimataifa, bali hali hiyo ingeweza kuwavuta mapromota wengine waKimataifa kuangalia kwa jicho la makini zaidi waimbaji wa Tanzania. Blog hii inaona ni vyema ingeongelea matukio mbalimbali ya wanamuziki wa Tanzania na vituko vyao jinsi vinavyowakosesha bahati wao na wadau wengine.
1. Mwanamuziki wetu mmoja maarufu alikuwa kapewa nafasi ya kurekodi katika studio moja wakati yuko katika tour huko Ulaya, akawa kakaribishwa katika nyumba ya Mtanzania fulani apumzike kungoja muda wa kwenda studio, kwa vile alikuwa peke yake katika nyumba alianza kunywa kila kila pombe aliyoiona humo ndani, bia za kopo za 7.5%alcohol katoni zima alimaliza peke yake, pombe kali aina mbalimbali alizigida, hatimae akazimika. Wenyeji wake walipofika kumchukua kwenda studio ilishindikana maana kila njia waliojitahidi kumsaidia azinduke ilishindikana ukawa ndo mwisho wa mpango wa kumrekodi hu…