Skip to main content

Posts

Showing posts from January 16, 2013

VANESSA MDEE ANANIKUMBUSHA MBALI

Sauti ya Vanessa Mdee ni mpya katika anga la muziki Tanzania, kwangu mimi ni ushahidi mwingine kuwa kipaji huwa kinatembea katika familia. Kwa kweli kilichonifanya nitake kusikilizamuziki wa huyu binti ni jina hili la Mdee. Mwaka 1972 nilijiunga na Chuo cha UalimuKleruu Iringa, pale chuoni kulikuwa na magitaa mapya kabisa, hiyo ilisababisha wote tuliokuwa wapiga magitaa kujenga urafiki na kukusanyikakila jioni kwenye kachumba kadogo na kufanya mazoezi, kwa kuwa chuo kilikuwa tayari kina mwaka mmoja tulikuta tayari wananchuo waliotangulia walikuwa wameanzisha bendi, na hapo ndipo nikamuona kwa mara ya kwanza mtengeneza filamu mashuhuri kutoka Tanga Kassim El  Siagi akiwa anapiga gitaa la solo. Kati ya wanachuo tulioingia mwaka huo pia alikuweko mmoja aliyeitwa Yusuph Mdee. Tulipatana mara moja baada ya kujiona wote tunapenda muziki aina moja, haraka tukafanya mpango mpaka kuweza kuishi katika chumba kimoja na magitaa yetu, tulipenda kupiga na kuimba muziki uliokuwa maarufu wakati huo, …

Mazishi ya mwanamuziki Lamania Shaaban kuwa kesho Tandika Maguruwe

Mkurugenzi, na mwanamuziki wa East African Melody Modern Taarab, Lamania Shaaban amefarika usiku wa kuamkia leo akiwa usingizini. Lamania alikuwa mpiga gitaa na mtunzi mzuri wa muziki wa Taarab, na atakumbukwa kwa tungo zake kama 'Utalijua Jiji'.
Marehemu alianza kuugua kiasai cha miaka minne iliyopita baada ya kupata stroke iliyomuweka kitandani kwa muda mrefu sana, karibuni alianza kuwa na nafuu kiasi cha kuweza kuhudhuria Ibada kwenye Msikiti uliokuwa karibu na kwake. Lakini Mungu amempenda zaidi na amefariki leo.
Marehemu atazikwa Tandika Maguruwe, baada ya Ibada za mwisho katika Msikiti wa Sheikh Kilembe kesho saa 7 mchana. Msiba uko Tandika Maguruwe, Mtaa wa Muwale.