Thursday, July 31, 2014

KUTAKAPOKUCHA KUWA MADUKANI 14/08/2014


Kutakapokucha ni filamu inayohadithia mkasa ya kiongozi mmoja aliyejiona Mungu mtu.  Akajitahidi kila njia kutaka kuhakikisha kuwa anabaki katika madaraka, lakini kulipokucha………….!!!!!!!!!!!!!!

MALUMBANO YA HOJA ITV..TRA YALAUMIWA KUHUSU UTEKELEZAJI WA SHERIA YA STIKA

Katika kipindi cha malumbano ya Hoja ambacho kinarushwa na ITV  kila Alhamisi baada ya taarifa ya habari ya saa 2 usiku wiki hii mada ilikuwa Wizi wa kazi za wasanii nini kifanyike? Wasanii wa Muziki na Filamu walikuweko na pia walikuweko maafisa kutoka TRA na Mtendaji Mkuu wa COSOTA. Jambo ambalo lilishikiwa bango na wengi walioongea ni mapungufu ya utekelezaji wa sheria ya kubandika stika ya TRA katika kazi za filamu na muziki. Producers wa kazi za filamu waliweza kuonyesha hasira zao kwa kutoa mifano ya kutokutekelezewa taratibu za kuziwa stika kwa muda na hata kukutwa kwa stika za TRA katika kazi ambazo n feki. Wengi wa waliozungumza walionekanakutokuridhishwa na taratibu hizo za TRA. Ukosefu wa stika katika miji mingine ulionyesha kuwa TRA ilikuwa ikichukulia biashara ya filamu na muziki kwa Dar es Salaam tu. Wasanii pia walionyesha kukerwa kwao na , sentensi ya kuwa sanaa inarasimishwa, na kuuliza je kulipishwa kodi ndio kurasimishwa? Bila serikali kutoa mchango wake wa ziada katika tasnia hizi? Swala jingine lililozungumziwa ni kukwepa kulipa mirabaha kwa vyombo vya utangazaji ambapo TBC ililaumiwa kuwa iko kimya japo yenyewe ndio chombo cha Taifa. Kulizungumziwa pia swala la mikataba kati ya wasambazaji na Producers, japo kulionekana na upungufu wa uelewa kwa kudhania kuwa wasanii huwa wanaingia mikataba na wasambazaji, jambo ambalo halipo. Kwa ujumla kipindi kingekuwa kizuri zaidi kma kungepewa muda tofauti kati ya wasanii wa filamu na wasanii wa muziki, kwani hatimae muda uliisha bila kuonekana njia yoyote ya kutatua tatizo la wizi wa kazi za sanaa.

HONGERA SANA DIAMOND....

Diamond akiwaonyesha mashabiki wake tuzo aliyoipata Marekani wiki iliyopita....Hongera sana

LADY JD NA DIAMOND WASHINDA TUZO YA AFRIMMA...IJUE AFRIMMA


AFRICAN MUZIK MAGAZINE AWARDS (AFRIMMA) ni Tuzo lilnalohusu watu weusi hasa wale ambao ni Waafrika waliohamia Magharibi. Ni Tuzo inayoangalia aina zote za muziki ukiwemo Afrobeats, Assiko, Bongoflava, Decale, Funana, Genge, Highlife, Hiplife, Kwaito, Lingala and Soukous na kadhalika. Kutokana na muziki wa Afrika kushika kasi katika kuingia kutambuliwa rasmi duniani, AFRIMMA waliona watengeneze jukwaa la kuwatambua wasanii wa Afrika katika nyanja ya muziki,  na katika kufanya hivyo kuwa na usiku ambao wasanii mbalimbali makini wa Afrika huwa pamoja na kufurahi. Kwa mara ya kwanza tuzo hizo zimefanyika tarehe 26 July 2014 Eisemann Center Richardson Texas. Wanamuziki wa Tanzania Lady JD na Diamond waliweza kupata tuzo katika siku hiyo. Orodha nzima ya waliopata tuzo ni kama ifuatavyo:

Best DJ Africa 2014- Dj Black (Ghana)
Best African DJ USA 2014 – Dj Josh (Kenya)
Best Video of the Year 2014- Flavour (Nigeria)
Best Male East Africa 2014- Diamond (Tanzania)
Best Male West Africa 2014- Davido (Nigeria)
Best Female East Africa 2014- Lady Jaydee (Tanzania)
Best Female West Africa 2014 – Tiwa Savage (Nigeria)
Best Male Central Africa 2014 – Fally Pupa (Congo)
Best Female Central Africa 2014- Gasha ( Cameroon)
Best Male Southern Africa 2014- Khuli Chana (South Africa)
Best African Group 2014- P-square (Nigeria)
Best Male Diaspora 2014- Fuse ODG (Ghana)
Best Female Diaspora 2014- Les Nubians (Cameroon)
Best Female Southern Africa 2014- Zahara (South Africa)
Best Dancehall Artist 2014 – Timaya (Nigeria)
Best Dance in a Video 2014- Iyanya (Lekwa Ukwu) (Nigeria)
Best Gospel Artiste 2014- Bahati (Kenya)
Best Traditional Artist 2014- Flavour (Nigeria)
Best Newcomer 2014- Stanley Enow (Cameroon)
Best Video Director 2014- Ogopa Dj’s (Kenya)
Music Producer of the year 2014- Dj Oskido (South Africa)
Best Dance Group 2014- Imagineto (Nigeria)
Best Rap Act 2014- Sarkodie (Ghana)
Best Collaboration 2014- Mafikizolo ft Uhuru (Khona) (South Africa)
Song of the Year 2014- Kcee (Nigeria)
Artist of the Year 2014- Davido (Nigeria)
Leadership in Music Award 2014- 2face Idibia
Legendary Award 2014- Yvonne Chaka Chaka
Transformational Leadership Award 2014- Chief Dr. Godswill Akpabio