MALUMBANO YA HOJA ITV..TRA YALAUMIWA KUHUSU UTEKELEZAJI WA SHERIA YA STIKA

Katika kipindi cha malumbano ya Hoja ambacho kinarushwa na ITV  kila Alhamisi baada ya taarifa ya habari ya saa 2 usiku wiki hii mada ilikuwa Wizi wa kazi za wasanii nini kifanyike? Wasanii wa Muziki na Filamu walikuweko na pia walikuweko maafisa kutoka TRA na Mtendaji Mkuu wa COSOTA. Jambo ambalo lilishikiwa bango na wengi walioongea ni mapungufu ya utekelezaji wa sheria ya kubandika stika ya TRA katika kazi za filamu na muziki. Producers wa kazi za filamu waliweza kuonyesha hasira zao kwa kutoa mifano ya kutokutekelezewa taratibu za kuziwa stika kwa muda na hata kukutwa kwa stika za TRA katika kazi ambazo n feki. Wengi wa waliozungumza walionekanakutokuridhishwa na taratibu hizo za TRA. Ukosefu wa stika katika miji mingine ulionyesha kuwa TRA ilikuwa ikichukulia biashara ya filamu na muziki kwa Dar es Salaam tu. Wasanii pia walionyesha kukerwa kwao na , sentensi ya kuwa sanaa inarasimishwa, na kuuliza je kulipishwa kodi ndio kurasimishwa? Bila serikali kutoa mchango wake wa ziada katika tasnia hizi? Swala jingine lililozungumziwa ni kukwepa kulipa mirabaha kwa vyombo vya utangazaji ambapo TBC ililaumiwa kuwa iko kimya japo yenyewe ndio chombo cha Taifa. Kulizungumziwa pia swala la mikataba kati ya wasambazaji na Producers, japo kulionekana na upungufu wa uelewa kwa kudhania kuwa wasanii huwa wanaingia mikataba na wasambazaji, jambo ambalo halipo. Kwa ujumla kipindi kingekuwa kizuri zaidi kma kungepewa muda tofauti kati ya wasanii wa filamu na wasanii wa muziki, kwani hatimae muda uliisha bila kuonekana njia yoyote ya kutatua tatizo la wizi wa kazi za sanaa.

Comments