Skip to main content

Posts

Showing posts from January 30, 2013

MASHAUZI CLASSIC WAKIWA GARDEN BREEZE BAR MAGOMENI

Katika kile kiota kipya cha burudani pale Magomeni, kwenye kituo cha Magomeni Hospitali, chenye jina Garden breeze Bar leo nimewakuta Mashauzi Classic Modern Taarab, watu wengi waliojaa katika onyesho hilo ambalo halina kiingilio, walionekana haswa wanafurahia burudani iliyokuwa ikitolewa na kundi hilo. Picha za matukio hapa chini. Ijumaa kuanzaia saa kumi na mbili watakuwepo 5 Star Modern Taarb, na Jumapili, Extra Bongo wako hapo muda kama huohuo.
Lady In Red 2013 Upgraded yatambulishwa rasmi

Lady In Red 2013 Upgraded, leo imetambulishwa rasmi kwa vyombo vya habari katika ukumbi waNyumbani Lounge. Mkurugenzi Mtendaji wa Lady In Red Bi Asya Khamsini alitambulisha wafadhili kadhaa waliokuwepo katika ukumbi huo, pia models na Designers watakao shiriki katika Fashion show hiyo itakayofanyika tarehe 9 February 2013 katika hotel ya Serena. Kwa maelezo ya Asya, show hiyo itakuwa na Designers wengi wapya na wachache wakongwe, hii ni makusudi ili kuweza kuwaingiza designers wapya katika ulimwengu wa designers. Katika siku hiyo pia kutakuweko na mnada wa kukusanya fedha kwa ajili ya kuendelea kituo cha waathirika wa madawa ya kulevya kilichoko Rufiji.