Bi Asya Khamsini |
Lady In Red 2013 Upgraded, leo imetambulishwa rasmi kwa
vyombo vya habari katika ukumbi wa
Nyumbani Lounge. Mkurugenzi Mtendaji wa Lady In Red Bi Asya Khamsini
alitambulisha wafadhili kadhaa waliokuwepo katika ukumbi huo, pia models na
Designers watakao shiriki katika Fashion show hiyo itakayofanyika tarehe 9 February
2013 katika hotel ya Serena.
Kwa maelezo ya Asya, show hiyo itakuwa na Designers wengi
wapya na wachache wakongwe, hii ni makusudi ili kuweza kuwaingiza designers
wapya katika ulimwengu wa designers. Katika siku hiyo pia kutakuweko na mnada
wa kukusanya fedha kwa ajili ya kuendelea kituo cha waathirika wa madawa ya
kulevya kilichoko Rufiji.
Comments