Wednesday, March 29, 2017

WANAMUZIKI KARIBUNI KUSHIRIKI TAMASHA LA MUZIKI LA KARIBU MUSIC FESTIVAL 2017


The Karibu Music Festival (KMF) yaja tena kwa mara ya nne katika mji wa Bagamoyo. Mwaka huu Tamasha hilo litakuwepo kuanzia Ijumaa tarehe 3 hadi Jumapili tarehe 5 Novemba.. Mwaka huu kunategemewa kuweko kwa wanamuziki kutoka  nchi mbalimbali za Afrika, Ulaya.Amerika na Asia, ambao watafanya maonyesho na pia kuendesha warsha mbalimbali. Wanaotaka kushiriki maombi yanapokelewa mpaka tarehe 31 mwezi Agosti 2017, wanaotaka kushiriki wanashauriwa kuwahi kutuma maombi. Wasanii kutoka Tanzania wanatapata posho kiasi , wakati wasanii kutoka nje watajitegemea kwa usafiri wa kuja mpaka Dar na huku watapewa malaziusafiri wa ndani na posho.Maswali yote kuhusu tamasha hili yatumwe info@karibumusic.org

KMF inatayarishwa na  Karibu Cultural Promotions Organisation kwa ushirikiano na  Legendary Music. Watayarishaji wanalenga katika kutoa mchango katika kukuza muziki wa Afrika na kujenga mahusiano kati ya washiriki. Tamasha litafanyika katika viwanja vyenye ukubwa wa hekta 200 vilivyo eneo la chuo cha sanaa cha TASUBA Tamasha ni wazi kwa kila aina ya muziki, uwe wa kiasili au wa kisasa kama vile Pop, rock, reggae, hip hop, jazz, country, electronic na aina nyingine za muziki. Kujaza maombi kwa mtandao ingia HAPA

Mwaka jana Tamasha lilikuwa na washiriki kama The CITY band na Afro-jazz artist Siphokazi (Afrika ya Kusini), Nkwali (Zimbabwe), Cie Art Dic (Togo), kundi la ngoma za kiasili Twekembe Performers (Uganda),  Third Hand Music band (Kenya),  Karakeeb(Misri). Na kutoka Tanzania washiriki walikuwemo pia Inafrika Band. Kwa kufwatilia maendeleo ya tamasha hili pita  official website , pia  Twitter.

MWITO KWA WASANII KUSHIRIKI TAMASHA LA SANAA UGANDA


JE,  unataka kushiriki katika tamasha la Bayimba International Festival, ambalo litafanyika tarehe 15-17 September 2017  Kampala, Uganda?
Tamasha la mwaka huu litakuwa ni la kumi. Ni tamasha ambalo linajumuisha muziki, dansa, maonyesho jukwaani, filamu, vichekesho, mashahiri, na sanaa za maonyesho. Wanaohitaji kushiriki ni muhimu kuwa wameshajaza fomu zao na kutuma ifikapo April 30. Katika tamasha la mwaka jana walikuweko wasanii wa Hiphop kama  Akua Naru kutoka Ghana, Tribute ‘Birdie’ Mboweni toka Afrika ya kusini, bibie wa Kiganda ambae ni mpiga saxaphone wa mahadhi ya soul Mo Roots, kundi la Reggae toka Kenya Gravittii Band, na wengine wengi. Kutakuwepo na malipo kidogo kwa washiriki toka nje ya Uganda, japo washiriki wanashauriwa kutafuta njia za kulipia gharama za usafiri, viza na bima mbalimbali. Barua ya utambulisho itatolewa mara utakapokubaliwa kushiriki ili ikusaidie kutafuta ufadhili. Wanaotaka kushiriki wanatakiwa watoe taarifa zifuatazo,
·     Fomu ya ushiriki na kupitia bayimbafestival.com
·     Maelezo mafupi ya wasanii yasiyozidi maneno 800 na picha ya karibuni 
·     Nakala ya kazi yako, kama ni muziki au filamu kazi moja au mbili kwenye CD, DVD or mp3.
·     Mahitaji yako ya vifaa (technical rider/data sheet)
Watayarishaji watawajibu mapema waliofanikiwa.Fomu za maombi zinapatikana pia  HAPA

APPLY FOR THE BAYIMBA INTERNATIONAL FESTIVAL


Artists can now apply to perform at the three-day Bayimba International Festival, which will be held on 15-17 September 2017 in Kampala, Uganda. For more details on the Festival continue here.....