JE, unataka kushiriki katika tamasha la Bayimba
International Festival, ambalo litafanyika tarehe 15-17 September 2017 Kampala, Uganda?
Tamasha la
mwaka huu litakuwa ni la kumi. Ni tamasha ambalo linajumuisha muziki, dansa,
maonyesho jukwaani, filamu, vichekesho, mashahiri, na sanaa za maonyesho.
Wanaohitaji kushiriki ni muhimu kuwa wameshajaza fomu zao na kutuma ifikapo
April 30. Katika tamasha la mwaka jana walikuweko wasanii wa Hiphop kama Akua Naru kutoka Ghana, Tribute
‘Birdie’ Mboweni toka Afrika ya kusini, bibie wa Kiganda ambae ni mpiga
saxaphone wa mahadhi ya soul Mo Roots, kundi la Reggae toka Kenya Gravittii
Band, na wengine wengi. Kutakuwepo na malipo kidogo kwa washiriki toka nje ya
Uganda, japo washiriki wanashauriwa kutafuta njia za kulipia gharama za
usafiri, viza na bima mbalimbali. Barua ya utambulisho itatolewa mara
utakapokubaliwa kushiriki ili ikusaidie kutafuta ufadhili. Wanaotaka kushiriki
wanatakiwa watoe taarifa zifuatazo,
·
Fomu ya
ushiriki na kupitia bayimbafestival.com
·
Maelezo mafupi ya wasanii yasiyozidi maneno 800 na
picha ya karibuni
·
Nakala ya kazi yako, kama ni muziki au filamu kazi
moja au mbili kwenye CD, DVD or mp3.
·
Mahitaji yako ya vifaa (technical rider/data sheet)
Watayarishaji
watawajibu mapema waliofanikiwa.Fomu za maombi zinapatikana pia HAPA
Comments