The Karibu
Music Festival (KMF) yaja tena kwa mara ya nne katika mji wa Bagamoyo.
Mwaka huu Tamasha hilo litakuwepo kuanzia Ijumaa tarehe 3 hadi Jumapili tarehe
5 Novemba.. Mwaka huu kunategemewa kuweko kwa wanamuziki kutoka nchi mbalimbali za Afrika,
Ulaya.Amerika na Asia, ambao watafanya maonyesho na pia kuendesha warsha
mbalimbali. Wanaotaka kushiriki maombi yanapokelewa mpaka tarehe 31 mwezi Agosti
2017, wanaotaka kushiriki wanashauriwa kuwahi kutuma maombi. Wasanii kutoka
Tanzania wanatapata posho kiasi , wakati wasanii kutoka nje watajitegemea kwa
usafiri wa kuja mpaka Dar na huku watapewa malaziusafiri wa ndani na
posho.Maswali yote kuhusu tamasha hili yatumwe info@karibumusic.org
KMF inatayarishwa na Karibu Cultural Promotions Organisation kwa
ushirikiano na Legendary
Music. Watayarishaji wanalenga katika kutoa mchango katika kukuza muziki wa
Afrika na kujenga mahusiano kati ya washiriki. Tamasha litafanyika katika
viwanja vyenye ukubwa wa hekta 200 vilivyo eneo la chuo cha sanaa cha TASUBA
Tamasha ni wazi kwa kila aina ya muziki, uwe wa kiasili au wa kisasa kama vile Pop,
rock, reggae, hip hop, jazz, country, electronic na aina nyingine za muziki.
Kujaza maombi kwa mtandao ingia HAPA
Mwaka jana Tamasha lilikuwa
na washiriki kama The CITY band na Afro-jazz artist Siphokazi (Afrika ya
Kusini), Nkwali (Zimbabwe), Cie Art Dic (Togo), kundi la ngoma za kiasili
Twekembe Performers (Uganda), Third Hand Music band (Kenya), Karakeeb(Misri). Na kutoka Tanzania washiriki walikuwemo pia
Inafrika Band. Kwa kufwatilia maendeleo ya tamasha hili pita official website ,
pia Twitter.
Comments