Monday, June 13, 2011

Carola Kinasha Sweet Eazy Ijumaa hii


Mwanamuziki muimbaji mahiri Carola Kinasha atakuwa katika ukumbi wa Sweet Eazy ( Oysterbay, Dar es Salaam), wiki hii siku ya Ijumaa 17 June 2011. Carola ambaye ni mwanamuziki wa miaka mingi aliyewahi kupitia vikundi kama Watafiti, Shada Group na bendi ya kimataifa iliyoluwa na wapigaji akinamama watupu Women Voices ambayo ilifanywa maonyesho katika nchi mballimbali duniani, ni mwimbaji ambaye ni burudani kumsikiliza. Usikose onyesho hili. Kwa maelezo zaidi piga simu +255 777461911 Kwame Mchauru. Au bonyeza hapa

Wanamuziki wakongwe mazoezini


Kundi la wanamuziki wenye umri zaidi ya miaka 50, wamekuwa katika mazoezi makali tayari kwa kutoa album ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa nchi yetu, na kufanya maonyesho ya muziki. Kundi hili la wanamuziki likiendeleza wazo lililoanza mwaka jana  baada ya wanamuziki kadhaa kufanya onyesho moja katika ukumbi wa Karimjee. Onyesho hilo ambalo lilikimbiwa na wafadhili katika dakika ya mwisho liliendelea kufanyika kwa mafanikio na kuongeza nia ya wanamuziki kufanya maonyesho kama hayo kila mwaka. Baadhi ya wanamuziki ambao wamekuwa katika mazoezi hayo ni Waziri Ally’ Kissinger’, Juma Ubao’King Makusa’, Kikumbi Wanzampango ‘King Kiki’, Hamza Kalala ‘Komando’, Mafumu Bilali Bombenga’Super Sax’, Kanku Kelly’King of Stage’, Akuliake Salehe’ King Maluu’, Juma Omari’Disco’, Kasongo Mpinda Clayton, Kabeya Badu, John Kitime, Andy Swebe’Ambassador, Mohamed Mrisho ‘Moddy’, Juma Sangula, Matei Joseph, Abdul Alvador 'Father Kidevu' na wengineo wengi.
Pamoja na kutunga nyimbo mpya pia kumekuweko na  mazoezi ya nyimbo ambazo wanamuziki hao walizipiga wakiwa katika bendi mbalimbali hapa nchini, mazoezi haya yamekuwa yanatembelewa na watangazaji wa vyombo mbalimbali na wasanii wa kutoka fani mbalimbali, kweli hapa ni mkusanyiko wa wakongwe.


Abou Mwinchumu

Akuliake Salehe 'King Maluu'

Kasongo Mpinda na King Kiki

Maluu katika pozi, wanaita swaga siku hizi


Kabeya Badu na Kasongo Mpinda


Hamza Kalala 'Komando'

Andy Swebe'Ambassador'

Lady- version ya Mark Band

Ilikuwa raha kuwepo katika ukumbi wa Sea Cliff wakati bendi hii ikipiga hebu pata vionjo na uweze kupata ushahidi mwingine wa uwezo wa wanamuziki wa Tanzania, japo kuna bidii za kufanya kuwa Tanzania hakuna wanamuziki wa maana.

TOT Taarab wakiwa Copa Cabana

Mrembo Mwasiti alikuwa wa kwanza kupanda jukwaani katika onyesho la jana
Ukumbi wa Copa Cabana Mwananyamala huwa na shamrashamra kila Jumapili usiku kwa kuwa kundi zima la TOT Taarab hufanya maonyesho mahali hapa. Ukumbi huu ambao awali ulijulikana kama Wami Bar, umefanyiwa ukarabati mkubwa na kuupa hali ya kuwa kama kumbi maarufu za gharama ambazo hutajwa kila mara katika vyombo vya habari. Ngumu kuhadithia raha zilizopo hapa baada ya saa 6 usiku ni kujionea mwenyeweAbdul Misambano kati ya wanamuziki walioitia sura mpya fani ya taarab


Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...