Skip to main content

Posts

Showing posts from October 8, 2012

HUU NI MUZIKI AU KUNA KITU KINGINE?

Baada ya kipindi kirefu ambapo zimekuwa zikienea picha za wasanii wa kike wakiwa nusu watupu jukwaani, sasa picha ambazo zinadaiwa ni za wasanii wa kiume wakijitahidi tena kwa makusudi kuwaiga dada zao zimeanza kuibuka. Ni ngumu kuelezea nini huwa kinapita katika vichwa vya wasanii kama hawa kwani kilichowapelekea kutunga staili kama hii juu pichani wanakijua wao tu. Lakini ni ukweli usiopingika kuwa haya ni matokeo ya malezi.  Kuna malezi ya wazazi na baadae malezi ya jamii. Ni wazi kuna tatizo kubwa katika malezi aidha kutoka kwa wazazi au kutoka kwa jamii.
Kuna wanamuziki wawili ambao waliwahi kurekodi nyimbo ambazo mashahiri yake yalikuwa na 'matusi' ndani yake. Mmoja wa wasanii hao alisaidiwa na MAMA YAKE MZAZI kutunga mashahiri hayo, kwa tuliye kuwa tukiifahamu historia ya mama yake hatukushangazwa na habari ile, kwani alikuwa akishinda baa toka mchana na mwanae huyo wakati mdogo. Mwingine alitunga wimbo wa matusi ambao hata kusambazwa ilishindikana lakini kuna taarifa…

MAONYESHO YA KWANZA YA KATUNI KATIKA UKUMBI WA ALLIANCE FRANCE

Msanii Simon Regis, ambae anae chora katuni katika Magazeti ya Mtanzania na The African leo amezindua maonyesho ya kazi katika ukumbi ulioko katika maeneo ya Alliance France- Kituo cha Utamaduni wa Kifaransa. Maonyesho haya yataendelea kwa wiki moja. Hii ni mara ya kwanza kwa kituo hicho kuwa na maonyesho ya katuni