Friday, May 31, 2013

KUTOKA KWA DJ CHOKA>>>YAH: MICHANGO YA MAANDALIZI YA MAZISHI YA ALBERT MANGWEHA


Kamati ya maandalizi ya msiba / mazishi ya msanii ndugu yetu Albert Kenneth Mangweha inapenda kutoa taarifa ya mchakati unaoendelea wa maandalizi ya mazishi, Kamati inahitaji michango yenu kwa ajili ya kufanikisha mazishi pale mwili wa marehemu utakapofika nchini Tanzani,kuanzia kuagwa kwa marehemu shughuli itakayofanyika jijini Dar es Salaam na kusafirishwa mjini Morogoro eneo la Kihonda kwa ajili ya Maziko.
Kusafirisha mwili wa marehemu pekee ni dola za kimarekani elfu sita gharama hizi zimetolewa na Clouds Media Group lakini vilevile kampuni ya Bongo records na Push Mobile kila moja imetoa shilingi milioni tano, EMasters wametoa Tenti 20,viti 1500 na gharama za uwanja wa Leaders pamoja na Mabasi Madogo aina ya coster 5 , Miraji Kikwete ambae yeye amejitolea kuprint tshirt 200 kwa familia na kamati, Samaki samaki wametoa Milioni Moja na Laki tano,skylyte Band wao wametoa gari ambalo litaupokea mwili wa Marehemu na kuusafirisha mpaka Morogoro,

Kwa wale wanaoweza kuchangia kupitia mitandao ya simu tuma kwa kaka wa marehemu Kenneth Mangweha namba zifuatazo:

Tigopesa - +255 717 553905
MPESA - +255 754 967738

Jina la akaunti: Kenneth B Mangweha
Namba ya akaunti: 2012505840
Benki: NMB

Tukitegemea ushirikiano wenu tunatanguliza shukrani za dhati

RATIBA YA TARATIBU ZA KUAGA MWILI WA ALBERT MANGWEA

Mwili wa marehemu Albert Mangwea unatarajiwa kuwasili kesho Jumamosi kwa ndege ya South African Airlines, ukitokea nchini Afrika ya kusini.

Mwili utapelekwa moja kwa moja katika hospitali ya muhimbili kuhifadhiwa. Clouds Media Group wamegharamia usafirishaji wa mwili wa msanii huyo kutoka South Africa mpaka hapa nyumbani.

Jumapili asubuhi, kuanzia saa mbili, mwili wa Albert Mangwea utakuwa unaagwa  katika viwanja vya Leaders Club, na hapa kampuni ya Entertainment Masters itaratibu zoezi hilo. Baada ya mwili kuagwa, safari ya kumsindikiza Albert Mangwea kuelekea kwenye maziko itanza, na hii itakuwa ni kuelekea Morogoro. Mwili wa Mangwea utazikwa Jumatatu katika eneo la Kihonda, mkoani Morogoro.
  Kampuni nyingine zilizotoa mchango wa mazishi ni Push Mobile shilingi Milioni 5, na Bongo records shilingi  Milioni 5IVORY BAND YAPANIA KUPAA KATIKA ANGA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA

Ijumaa hii na kila Ijumaa ni siku ya raha na starehe kwa wakazi wa Tabata na vitongoji vyake, maana mara tu baada ya jua kuzama kiota maaru...