Posted by
jfk
on
- Get link
- X
- Other Apps
Kamati ya maandalizi ya msiba / mazishi ya msanii ndugu yetu Albert
Kenneth Mangweha inapenda kutoa taarifa ya mchakati unaoendelea wa
maandalizi ya mazishi, Kamati inahitaji michango yenu kwa ajili ya
kufanikisha mazishi pale mwili wa marehemu utakapofika nchini
Tanzani,kuanzia kuagwa kwa marehemu shughuli itakayofanyika jijini Dar
es Salaam na kusafirishwa mjini Morogoro eneo la Kihonda kwa ajili ya
Maziko.
Kusafirisha mwili wa marehemu pekee ni dola za kimarekani
elfu sita gharama hizi zimetolewa na Clouds Media Group lakini vilevile
kampuni ya Bongo records na Push Mobile kila moja imetoa shilingi
milioni tano, EMasters wametoa Tenti 20,viti 1500 na gharama za uwanja
wa Leaders pamoja na Mabasi Madogo aina ya coster 5 , Miraji Kikwete
ambae yeye amejitolea kuprint tshirt 200 kwa familia na kamati, Samaki
samaki wametoa Milioni Moja na Laki tano,skylyte Band wao wametoa gari
ambalo litaupokea mwili wa Marehemu na kuusafirisha mpaka Morogoro,
Kwa wale wanaoweza kuchangia kupitia mitandao ya simu tuma kwa kaka wa marehemu Kenneth Mangweha namba zifuatazo:
Tigopesa - +255 717 553905
MPESA - +255 754 967738
Jina la akaunti: Kenneth B Mangweha
Namba ya akaunti: 2012505840
Benki: NMB
Tukitegemea ushirikiano wenu tunatanguliza shukrani za dhati
- Get link
- X
- Other Apps
Comments