RATIBA YA TARATIBU ZA KUAGA MWILI WA ALBERT MANGWEA

Mwili wa marehemu Albert Mangwea unatarajiwa kuwasili kesho Jumamosi kwa ndege ya South African Airlines, ukitokea nchini Afrika ya kusini.

Mwili utapelekwa moja kwa moja katika hospitali ya muhimbili kuhifadhiwa. Clouds Media Group wamegharamia usafirishaji wa mwili wa msanii huyo kutoka South Africa mpaka hapa nyumbani.

Jumapili asubuhi, kuanzia saa mbili, mwili wa Albert Mangwea utakuwa unaagwa  katika viwanja vya Leaders Club, na hapa kampuni ya Entertainment Masters itaratibu zoezi hilo. Baada ya mwili kuagwa, safari ya kumsindikiza Albert Mangwea kuelekea kwenye maziko itanza, na hii itakuwa ni kuelekea Morogoro. Mwili wa Mangwea utazikwa Jumatatu katika eneo la Kihonda, mkoani Morogoro.
  Kampuni nyingine zilizotoa mchango wa mazishi ni Push Mobile shilingi Milioni 5, na Bongo records shilingi  Milioni 5Comments