Skip to main content

Posts

Showing posts from May 15, 2013

UNAKARIBISHWA GOETHE INSTITUT KUONYESHA KIPAJI CHAKO

Goethe Institut yawakaribisha wasanii  24.05.2013, kuja kuonyesha vipaji vyao katika  OPEN STAGE NIGHT . Kila mtu anakaribishwa kuonyesha kipaji chake chochote. Ili kuijisajiri andika barua pepe au piga simu: intern@daressalaam.goethe.org, Tel.:  075 375 152  ueleze unachotaka kufanya na msaada wa vifaa utakavyohitaji, wanamuziki wanaweza kuja na vyombo vyao kiingilio bureeeeee GOETHE INSTITUT IKO UPANGA 

BARUA YA MHE. ZITTO KABWE

DR ABDALLAH KIGODA, Waziri wa Viwanda na BiasharaKuhusu: BIASHARA YA MIITO YA SIMU (RINGBACK TONES)
Kumekuwa na malalamiko makubwa sana kuhusu biashara ya mauzo ya nyimbo kamamiito kwenye simu. Malalamiko haya yalianzia kwa wasanii wenyewe na baadaye mimibinafsi niliwasilisha hoja zao Bungeni mwaka 2012. Hata hivyo, hadi sasa malalamikohaya bado hayajapatiwa ufumbuzi na hivyo wasanii kuendelea kunyonywa. Tatizokubwa katika biashara hii ni USIRI na UNYONYAJI kwa wasanii wa Tanzania. Suala la USIRI lipo Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Suala la Unyonyaji lipoWizara ya Viwanda na Biashara. USIRI
Biashara hii ya “Ring Back Tones” (RBT) hufanywa na Kampuni za simu (Networkproviders) kwa kununua maudhui kutoka wachuuzi (Content Providers) ambao naohuingia mikataba na Wasanii (Content Creators). Hakuna sheria yoyote au Kanuni hapa nchini inayoongoza biashara hii na hivyo“Network providers” na “Content Providers” kuwa watu pekee wenye taarifa zote zabiashara hii. Kampuni za simu …