BARUA YA MHE. ZITTO KABWE

DR ABDALLAH KIGODA, Waziri wa Viwanda na BiasharaKuhusu: BIASHARA YA MIITO YA SIMU (RINGBACK TONES)
Kumekuwa na malalamiko makubwa sana kuhusu biashara ya mauzo ya nyimbo kamamiito kwenye simu. Malalamiko haya yalianzia kwa wasanii wenyewe na baadaye mimibinafsi niliwasilisha hoja zao Bungeni mwaka 2012. Hata hivyo, hadi sasa malalamikohaya bado hayajapatiwa ufumbuzi na hivyo wasanii kuendelea kunyonywa. Tatizokubwa katika biashara hii ni USIRI na UNYONYAJI kwa wasanii wa Tanzania.
Suala la USIRI lipo Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Suala la Unyonyaji lipoWizara ya Viwanda na Biashara.
USIRI
Biashara hii ya “Ring Back Tones” (RBT) hufanywa na Kampuni za simu (Networkproviders) kwa kununua maudhui kutoka wachuuzi (Content Providers) ambao naohuingia mikataba na Wasanii (Content Creators). Hakuna sheria yoyote au Kanuni hapa nchini inayoongoza biashara hii na hivyo“Network providers” na “Content Providers” kuwa watu pekee wenye taarifa zote zabiashara hii. Kampuni za simu hujumuisha mapato ya biashara hii na mapato yake mengine (Not Ringfenced), hawatoi taarifa za manunuzi ya nyimbo (au ‘content’nyingine yeyote) kwa wadau na hasa wasanii.
Wachuuzi (Content Providers) naohawatoi taarifa za mauzo kwa wasanii na wanatumia uelewa mdogo wa wasaniikuwasainisha mikataba inayowanyonya. Matokeo yake ni kwamba msanii hupata kiasicha asilimia mbili tu (2.5%) ya mapato ghafi ya kazi yake. Hivi sasa biashara hiiinathamani (turnover) ya takribani shilingi 44 bilioni kwa mwaka.
Suluhisho: Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano iandike kanuni (regulations) zitakazolazimishamakampuni ya simu kuweka wazi mapato yatokanayo na biashara ya RBT (Miito yasimu) kila baada ya miezi 4 (disclosure rules). Kanuni hizi zielekeze makampuni kutoataarifa za mauzo kwa kila kazi (nyimbo/vichekesho etc.)
UNYONYAJI
Kutokana na usiri ulioelezwa hapo juu, wasanii wamekuwa wakinyonywa kimapato.Kwa mfano Msanii hulipwa mapato yatokanayo na ununuzi wa awali wa kazi yake(wimbo) katika mwezi (downloads).Lakini mapato yatokanayo na “subscriptions” ambapo mlaji hukatwa shilingi 30 kila sikumsanii hapati chochote. Hivyo katika mapato ya sh. 1,300 kila mwezi kwa kila mtejakwa kila wimbo, msanii hupata mgawo wake kutoka shilingi 400 tu za ‘downloads’ nandio maana wasanii wote nchini hupata 2.5% ya shilingi 44 bilioni zinazokusanywa naKampuni za Simu.
Nchini Marekani biashara ya miito ya simu (RBT) imetafsiriwa kama maonyesho (PublicPerformances) na hivyo “copyright Association” ya Marekani imeweka kiwango chachini cha mrahaba (royalty) ambacho msanii hulipwa. Marekani msanii hulipwa asilimia10 ya patoghafi linalozalishwa na kazi yake kama muito wa simu.
SULUHISHO
Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara iandike kanuni kwamba mauzo ya kaziza wasanii kama miito ya simu inachukuliwa kama ‘performance’ na kwamba Kampuniza simu zitalipa sio chini ya asilimia 12 (12%) ya mapato ghafi, ambapo asimilia 10%itakwenda kwa msanii na asilimia 2% COSOTA kwa ajili ya usimamizi na Ulinzi wa kaziza Wasanii.
HITIMISHO
Kanuni za Uwazi (disclosure rules) katika biashara hii ya ‘Ring Back Tones’ na mgawowa haki wa mapato (fair and just revenue share) ndio suluhisho endelevu na litakaloletatija kwa wasanii wa Tanzania na hata Serikali kukusanya mapato stahili. Kanuni(Regulations) zinazopendekezwa zianze kutumika kuanzia tarehe 1/7/2013
Kabwe Z. Zitto, Mb
Kigoma KaskaziniDodoma, 13 Mei 2013.

Comments