Skip to main content

Posts

Showing posts from January 4, 2013

WASANII HAWAJAJIPANGA KATIKA MFUMO WA STIKA ZA TRA....TATIZO LITAFUMUKA

MATANGAZO YA CD, DVD, NA VCD ZOTE NCHINI KUWA STEMPU MBILI ZA TRA YAMEANZA KURUSHWA KATIKA LUNINGA, YAKIELEKEZA KUANZA KUTEKELEZWA KWA SHERIA HII, JANUARI HII. USHAURI KWA WASANII NI LAZIMA KUJIULIZA MATOKEO YA KUTEKELEZWA KWA SHERIA HII NA KUJIPANGA ILI KULINDA MASLAHI YAO KATIKA MTIRIRIKO WA UTEKELEZAJI WA TARATIBU HIZI ZA SERIKALI KUKUSANYA KODI. Wasanii hawana chombo chochote ambacho kinalinda maslahi yao ya Hakimiliki kwa pamoja, chombo ambacho kingelinda haki zao nchini na pia kuingia katika makubaliano na vyombo vya nje ili kulinda haki zao nje ya nchi. Serikali imekwisha weka taratibu zake za kukusanya kodi kutoka kazi za muziki na filamu, japo hili kwa muda wote limekuwa likitangazwa kama ni njia ya kusaidia kulinda kazi za wasanii, bado haijaonyeshwa ni vipi kazi hizi zitalindwa. Tangazo linaloonyesha kuanza kuweka stempu kwenye kazi zote Januari, kiukweli halitekelezeki na kuanza kuleta maswali kwa nini serikali inatoa tamko ambalo halitaweza kutekelezwa. Utafiti wa kutosh…

WANAMUZIKI WATANZANIA WALIOKO JAPAN

Wanamuziki wetu Abbu Omar, Fresh Jumbe, Lister Elia wanatuwakilisha vizuri sana huko Japan hapa picha zao wakiwa kazini. Kazi njema jamani, halafu mrudi kurithisha vipaji.

Buriani Sajuki

Mamia ya watu wakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete walishiriki katika mazishi ya Sadick Juma Kilowoko SAJUKI leo katika makaburi ya Kisutu mjini Dar es salaam Pumzika kwa Amani Sajuki

HAKIMILIKI NI NINI? msanii jielewe

HAKIMILIKI KWA UFUPI SANA
Hakimiliki ni nini? Hakimiliki ni haki za kisheria anazopewa mtunzi na mbunifu katika kazi zake za utunzi na ubunifu. Hakimiliki huambatana na haki nyingine zinazoitwa Hakishiriki ambazo hulinda wale ambao huwezesha kufanikiwa kwa kazi za hakimiliki huonekana hadharani. Kama ni mchezo wa filamu waigizaji hulindwa na Hakishiriki wakati mtunzi wa script hulindwa na hakimiliki, katika muziki, Producers hulindwa na Hakishiriki mtunzi wa wimbo hulindwa na Hakimiliki, pia haki hizi huvilinda vyombo vya utangazaji katika haki za vipindi vyao. Hakimiliki hulinda aina nyingi za kazi kama vile; a.Kazi za kimaandishi (vitabu,hotuba,magazeti,novo, hadithi fupi na ndefu, mashahiri na kadhalika) b.Kazi za muziki (tungo za muziki zenye maneno na ala tupu, mashahiri ya muziki, ringtones za simu na kadhalika c.Kazi za kisanii (michoro, vibonzo, picha za rangi za maji, fotografia, za kuchonga, ufinyanzi, ususi na kadhalika)