WASANII HAWAJAJIPANGA KATIKA MFUMO WA STIKA ZA TRA....TATIZO LITAFUMUKA


MATANGAZO YA CD, DVD, NA VCD ZOTE NCHINI KUWA STEMPU MBILI ZA TRA YAMEANZA KURUSHWA KATIKA LUNINGA, YAKIELEKEZA KUANZA KUTEKELEZWA KWA SHERIA HII, JANUARI HII. USHAURI KWA WASANII NI LAZIMA KUJIULIZA MATOKEO YA KUTEKELEZWA KWA SHERIA HII NA KUJIPANGA ILI KULINDA MASLAHI YAO KATIKA MTIRIRIKO WA UTEKELEZAJI WA TARATIBU HIZI ZA SERIKALI KUKUSANYA KODI. Wasanii hawana chombo chochote ambacho kinalinda maslahi yao ya Hakimiliki kwa pamoja, chombo ambacho kingelinda haki zao nchini na pia kuingia katika makubaliano na vyombo vya nje ili kulinda haki zao nje ya nchi. Serikali imekwisha weka taratibu zake za kukusanya kodi kutoka kazi za muziki na filamu, japo hili kwa muda wote limekuwa likitangazwa kama ni njia ya kusaidia kulinda kazi za wasanii, bado haijaonyeshwa ni vipi kazi hizi zitalindwa. Tangazo linaloonyesha kuanza kuweka stempu kwenye kazi zote Januari, kiukweli halitekelezeki na kuanza kuleta maswali kwa nini serikali inatoa tamko ambalo halitaweza kutekelezwa. Utafiti wa kutosha haujafanywa, na elimu ya kutosha kwa wadau wote haijafanywa, mchanganyiko unaohakikisha kuwa lazima kutakuwa na fujo mbele. Kwanini kutengeneza mazingira ya fujo? Maelezo ya awali yalikuwa kazi mpya ndio zitaanza kuwa na stempu na kuwawezesha wafanya biashara kuondoa mali ya zamani na muda uliotolewa ni mpaka July, hili tangazo jipya lina lengo gani?

Comments