HAKIMILIKI KWA UFUPI SANA
Hakimiliki ni nini?
Hakimiliki ni haki za kisheria anazopewa mtunzi
na mbunifu katika kazi zake za utunzi na ubunifu. Hakimiliki huambatana na haki
nyingine zinazoitwa Hakishiriki ambazo hulinda wale ambao huwezesha kufanikiwa
kwa kazi za hakimiliki huonekana hadharani. Kama ni mchezo wa filamu waigizaji
hulindwa na Hakishiriki wakati mtunzi wa script hulindwa na hakimiliki, katika
muziki, Producers hulindwa na Hakishiriki mtunzi wa wimbo hulindwa na
Hakimiliki, pia haki hizi huvilinda vyombo vya utangazaji katika haki za
vipindi vyao.
Hakimiliki hulinda aina
nyingi za kazi kama vile;
a.
Kazi za kimaandishi (vitabu,hotuba,magazeti,novo, hadithi fupi na ndefu,
mashahiri na kadhalika)
b. Kazi za muziki (tungo za muziki zenye maneno na ala tupu,
mashahiri ya muziki, ringtones za simu na kadhalika
c. Kazi za kisanii (michoro, vibonzo, picha za rangi za maji,
fotografia, za kuchonga, ufinyanzi, ususi na kadhalika)
d. Sanaa za maonyesho (Michezo ya kuigiza ya jukwaani,operas na
kadhalika)
e. Filamu na kazi nyingine za multimedia (video, video
games,vipindi vya TV,cartoons, filamu nk)
f. Program za
kompyuta.
Kwa maelezo ya hapo juu utaweza kuona
kuona kuwa si kila msanii hulindwa na Hakimiliki, wengine haki zao zinalindwa
na Hakishiriki.
Hakimiliki hutoa haki za aina mbili.
i.
Moral rights- Haki za
kimaadili ambazo hulazimisha watumiaji kumtambua mtunzi katika kazi zake, kwa
mfano mtunzi wa kitabu kutajwa kwenye jalada la kitabu, au mcheza filamu
kutajwa jina lake mwisho au mwanzo wa filamu. Hki hizi huwezi kumpa mtu
mwingine.
ii.
Economic rights- hizi ni
haki zinazoleta faida za kiuchumi katika kazi ya mtunzi, na hizi ndio huleta
migogoro na kelele nyingi tunazozisikia kila siku kuhusu wasanii kuibiwa.
Economic
rights- Hizi ndizo haki ambazo huvunjwa sana na huonekana sana matokeo
kwani huwatajirisha wengine na wengine kuwatia umasikini. Haki hizi hutolewa
kwa mtunzi pekee (exclusive rights) na hivyo yeye huweza kuzitumia kwa njia
ambayo anaweza kuona inafaa katika kumuongezea kipato. Haki hizi ni kama
zifuatazo;
i.
kurudufu…kutengeneza nakala ambazo anaweza kuuza
ii.
kutafsiri kazi
iii.
kubadili matumizi ya kazi (km wimbo wa dansi kugeuzwa ringtone,
kitabu cha hadithi kuwa sinema na kadhalika)
iv.
Kuonyesha hadharani kazi (Exhibition au performance)
v.
Kusambaza kazi…kuuza kazi
vi.
Kutangaza katika vyombo vya utangazaji(Broadcasting)
vii.
Mawasiliano ya kazi (kwa kupitia intanet)
Mtunzi hukabidhi haki hizi kwa wasambazaji, ili wasambaze kazi
zake kwa makubaliano maalum, pasipokuweko na makubaliano hapo ndipo wizi wa
kazi za sanaa kwa njia ya Piracy hutendeka.
Kutokana
na mapato makubwa ambayo yanaweza kutokana na mapato ya Hakimiliki, kwa watunzi
na serikali, serikali pamoja na kuunda sheria za hakimiliki huwa na ofisi ya
serikali ya kuratibu uendeshwaji wa sera na shughuli za hakimiliki, hivyo ni muhimu kuwa na COPYRIGHT
OFFICE (Tanzania hatuna), ambayo yenyewe huratibu vyombo mbalimbali
vinavyohusika kwa njia moja au nyingine katika Hakimiliki.
Ili kulinda haki za wasanii wa muziki na filamu huwa kunakuweko vyama vya wadau vya hakimiliki, huwa kunakuweko na Performing Rights Societies ambazo hufuatilia matumizi ya hakimiliki kwa mfano katika matumizi kwenye Radio, TV, kumbi mbalimbali nakadhalika, halafu huweko Mechanical Rights Societies ambazo hufuatilia taratibu za mauzo ya kazi za sanaa.
Ili kulinda haki za wasanii wa muziki na filamu huwa kunakuweko vyama vya wadau vya hakimiliki, huwa kunakuweko na Performing Rights Societies ambazo hufuatilia matumizi ya hakimiliki kwa mfano katika matumizi kwenye Radio, TV, kumbi mbalimbali nakadhalika, halafu huweko Mechanical Rights Societies ambazo hufuatilia taratibu za mauzo ya kazi za sanaa.
Katika nchi yetu, Hakimiliki hulindwa kwa
maisha yote ya mtunzi na miaka hamsini baada ya kifo chake. Kwa ulinzi huu
mrefu, kila mara wanaouza masters waelewe wanauza pamoja haki hii, ambayo
ingewawezesha watoto wao na wajukuu zao kufaidi matunda yao. Mwalimu Nyerere
aliwahi kusema kuna wakulima wanakula mpaka mbegu……
25
Comments