Monday, February 20, 2012

Jahazi Modern Taarab

Pamoja na kuwa 'Mfalme ' hakuweko(yuko kwenye ziara ya kikazi Marekani), burudani ya Jahazi ilikuwa palepale katika ukumbi wa Travetine. Muziki ukiporomoshwa katika ile aina mpya ya 'taarab', watu walifurahi. Kitu kimoja kilichokuwa wazi,watu wengi zaidi walikuwa wakicheza nyimbo hizi za 'Taarab' kuliko katika 'dance bands' nyingi. Kitu ambacho ningeshauri wanamuziki wa bendi wafanye utafiti inakuwaje Taarab ambayo asili yake si kucheza, watu wanashiriki kucheza zaidi ya muziki wa dansi ambao nia yake ni watu wacheze.


FM Academia

Jana nilipita katika ukumbi wa New Msasani Club, hapo nimewakuta FM Academia wakiangusha show ya nguvu, iliyokuwa wazi ikiwakonga wapenzi wao. Ukumbi huu ambao awali ulikuwa ni wavumbi tupu, sasa umeendelea kufanyiwa ukarabati na kuongezeka ubora, huku Masebene yakiangushwa moja baada ya jingine na bendi hii ambayo inastahili sasa kuitwa kongwe. Big Up FM Academia

The B band

Kila Jumapili mchana Banana Zollo na B Band huwa pale Cine Club wakiporomosha variety kubwa ya muziki, kuanzia ule wa zamani maarufu kama zilipendwa, mpaka muziki ulioko katika chati za siku hizi. Wakisindikizwa na mkongwe na mmoja ya wapiga gitaa mahiri Tanzania Maneno Uvuruge B Band ina raha zake sana
Ashura Kitenge na Maneno Uvuruge

Michael


Idrisa Kunde

Daudi Ngedele

Goddy

Banana Zoro

Vasmo Onesmo

Ashura Kitenge

Anette Kushaba

All Mtama

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...