Wednesday, June 8, 2011

Kukaye Moto Band mwanamuziki wa Kitanzania Ujerumani


Kukaye Moto , ni bendi iliyoanzishwa na Arba Manillah mwaka 2004, Arba ambaye ametokea Iringa ameipa jina hilo bendi hii akitumia neno la Kihehe ‘Kukaye’ ambayo maana yake ni Nyumbani, na neno la Kiswahili moto. Hivyo jina la bendi kutafsiriwa kuwa Nyumbani Moto Band. Bendi hii yenye maskani Ujerumani ina wanamuziki kutoka pande mbalimbali za dunia. Imesharekodi album mbili ya kwanza Jua lile, na ya pili Waowao. Bendi inapiga mchanganyiko wa Afrobeat na Livangala. Livangala ikiwa ni ngoma ya Kihehe.  Ukitaka kusikia nyimbo za bendi hii bonyeza HAPA

Mpiga gitaa mpya atua Twanga

Selemani Shaibu
African Stars Band “Twanga Pepeta” imempata mpiga Gitaa la Solo na Rhythm ili kuziba pengo la Adolph Mbinga aliyeondolewa ndani ya Bendi.

Mpiga gitaa huyo ni  Selemani Shaibu aliwahi kupigia  bendi ya Akudo Impact.  Selemani anaungana na Miraji Shakashia, Godfrey Kanuti, Jojoo Jumanne na Hassan Kado, katika upande wa magitaa.Twanga Pepeta kwa sasa ipo kwenye matayarisho ya kukamilisha kurekodi nyimbo 4 ili kukamilisha albamu ya nyimbo sita itakayozinduliwa hapo baadae mwaka huu.

 Nyimbo zinazotarajiwa kurekodiwa ni “Dunia Daraja” uliotungwa na Charlz Baba,” Penzi la shemeji” uliotungwa na Mwinjuma Muumini, “Mtoto wa Mwisho” uliotungwa na Ramadhani Athumani au Dogo Rama na “Umenivika Umasikini”  wa Luizer Mbutu.

 Nyimbo hizi zitaunganishwa na nyingine mbili zilizorekodiwa hapo awali ambazo ni “Kiapo cha Mapenzi” uliotungwa na Saleh Kupaza na “Kauli” uliotungwa na Rogart Hegga wakati huo kabla ya kuhamia  Extra Bongo.Selemani Shaibu akiwa na Miraji Shakashia

Mtangazaji maarufu apata tuition ya kuimba

ajMtangazaji maarufu wa Clouds TV Sakina Lyoka, alipita katika kambi ya wanamuziki wakongwe katika mizunguko ya kutengeneza documentary ya mazoezi ya wanamuziki wakongwe, alipokuwa huko alipata tuition ya kuimba toka kwa wakongwe King Kiki, Kasongo Mpinda, Kanku Kelly na John Kitime


Twanga na Dully Sykes kuwa pamoja Jumapili 12 June, Mbaramwezi Beach

African Stars Band "Twanga Pepeta" inataraji kufanya onesho pamoja na msanii Dully Sykes siku ya Jumapili Juni 12, pale Mbalamwezi Beach. Onyesho hilo la aina yake litaanza saa nne asubuhi kwa kuwa  usiku Twanga Pepeta itakuwa katika ukumbi T.C.C Chang’ombe kama kawaida ambapo pia itawatambulisha vimwana kumi walioingia katika fainali za Kimwana wa Twanga Pepeta 2011


Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...