Kukaye Moto , ni bendi iliyoanzishwa na Arba Manillah mwaka 2004, Arba ambaye ametokea Iringa ameipa jina hilo bendi hii akitumia neno la Kihehe ‘Kukaye’ ambayo maana yake ni Nyumbani, na neno la Kiswahili moto. Hivyo jina la bendi kutafsiriwa kuwa Nyumbani Moto Band. Bendi hii yenye maskani Ujerumani ina wanamuziki kutoka pande mbalimbali za dunia. Imesharekodi album mbili ya kwanza Jua lile, na ya pili Waowao. Bendi inapiga mchanganyiko wa Afrobeat na Livangala. Livangala ikiwa ni ngoma ya Kihehe. Ukitaka kusikia nyimbo za bendi hii bonyeza HAPA
Comments