Selemani Shaibu |
African Stars Band “Twanga Pepeta” imempata mpiga Gitaa la Solo na Rhythm ili kuziba pengo la Adolph Mbinga aliyeondolewa ndani ya Bendi.
Mpiga gitaa huyo ni Selemani Shaibu aliwahi kupigia bendi ya Akudo Impact. Selemani anaungana na Miraji Shakashia, Godfrey Kanuti, Jojoo Jumanne na Hassan Kado, katika upande wa magitaa.
Twanga Pepeta kwa sasa ipo kwenye matayarisho ya kukamilisha kurekodi nyimbo 4 ili kukamilisha albamu ya nyimbo sita itakayozinduliwa hapo baadae mwaka huu.
Nyimbo zinazotarajiwa kurekodiwa ni “Dunia Daraja” uliotungwa na Charlz Baba,” Penzi la shemeji” uliotungwa na Mwinjuma Muumini, “Mtoto wa Mwisho” uliotungwa na Ramadhani Athumani au Dogo Rama na “Umenivika Umasikini” wa Luizer Mbutu.
Nyimbo hizi zitaunganishwa na nyingine mbili zilizorekodiwa hapo awali ambazo ni “Kiapo cha Mapenzi” uliotungwa na Saleh Kupaza na “Kauli” uliotungwa na Rogart Hegga wakati huo kabla ya kuhamia Extra Bongo.
Selemani Shaibu akiwa na Miraji Shakashia |
Comments