Skip to main content

Posts

Showing posts from February 10, 2013

LADY IN RED 2013 YAFANA

Usiku wa Lady in Red 2013, ulikuwa mtamu kama matangazo yalivyoahidi. Kulikuweko na matukio mbalimbali, yakiwemo maonyesho ya mavazi ya wabunifu (designers), models wazuri, sanaa mbalimbali , wakiongozwa na Kalunde Band ambayo ilikuwa moja ya wadhamini, pia alikuweko msanii Wanne star akiwa na wasanii wake, Baby Madaha. Nguo za aina mbalimbali zilionyeshwa na hatimae kukaweko na mnada mkubwa wa kukusanya fedha kwa ajili ya kituo cha vijana walioathirika na madawa ya kulevya katika wilaya ya Rufiji, ambapo gauni lililovaliwa na Redds Miss Tanzania lilinunuliwa kwa shilingi 2,500,000.00