Usiku wa Lady in Red 2013, ulikuwa mtamu kama matangazo yalivyoahidi. Kulikuweko na matukio mbalimbali, yakiwemo maonyesho ya mavazi ya wabunifu (designers), models wazuri, sanaa mbalimbali , wakiongozwa na Kalunde Band ambayo ilikuwa moja ya wadhamini, pia alikuweko msanii Wanne star akiwa na wasanii wake, Baby Madaha. Nguo za aina mbalimbali zilionyeshwa na hatimae kukaweko na mnada mkubwa wa kukusanya fedha kwa ajili ya kituo cha vijana walioathirika na madawa ya kulevya katika wilaya ya Rufiji, ambapo gauni lililovaliwa na Redds Miss Tanzania lilinunuliwa kwa shilingi 2,500,000.00
Gauni lililopigwa mnada kwa shilingi milioni 2.5 katika kuchangia kuendeleza kituo cha waathirika wa madawa ya kulevya |
Kinyago kilichopigwa mnada kwa ajili ya kuchangia kituo |
Picha iliyopigwa mnada |
Disgners na models |
Waimbaji walikuweko wa kila aina |
Asia Khamsini akiwa na mumewe. |
Comments